Home » » SAKATA LA MWANAFUNZI ALIYEFUTWA SHULE KWA MIMBA WANAHARAKATI WAIAGUKIA TAKUKURU

SAKATA LA MWANAFUNZI ALIYEFUTWA SHULE KWA MIMBA WANAHARAKATI WAIAGUKIA TAKUKURU


Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dk. Edward Hoseah.

ZIKIWA zimepita siku takribani mbili toka mtandao huu wa www.francisgodwin kwa kushirikiana na radio Country fm kupitia kipindi cha asubuhi Tulivu kuibua sakata la mwanafunzi wa shule ya Msingi Njiapanda kukutwa na ujauzito na uongozi wa shule hiyo kumfuta katika orodha ya wanafunzi wanaopaswa kufanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya msingi .wanaharakati mbali mbali wameibuka na kutaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kufuatilia sakata hilo ambalo linaonyesha kuwa na harufu ya rushwa ndani yake.

Mwanaharakati wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP ) Deo Temba kutoka jijini Dar es Salaam na Juma Nyumayo kutoka mkoa wa Ruvuma pamoja na mkuu wa kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake na watoto mkoani Iringa Jackson Gaso wamesema kuwa pamoja na uongozi wa shule hiyo ya Njiapanda kueleza jinsi suala hilo walivyolishughulikia ila bado kuna onyesha kuwepo na mazingira machafu ya rushwa ambayo yamepenyeza katika sakata hilo.

Hivyo wametaka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Iringa kuweza kutoka ofisini na kwenda katika shule hiyo ya Msingi Njiapanda ili kufuatilia sakata hilo kwa karibu zaidi.

Alisema Nyumayo kuwa vitendo vya watu kuwapa ujauzito wanafunzi na kumaliza nje ya vyombo vya sheria vimezidi kuongezeka na kuwa katika suala hilo la shule ya Msingi Njiapanda na lile la shule ya Sekondari Mlandege ni vema serikali ya mkoa wa Iringa vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama na TAKUKURU kuweza kufuatilia zaidi utata huo ambao umesababishwa na mtu mmoja ambaye ni dereva wa Lori anayesadikika bado yupo katika mji wa Iringa akiendelea kuhonga fedha kwa wazazi ,uongozi wa serikali ya mtaa wa Isakalilo na walimu ili kuendelea kulindwa .

Wakati kwa upande wake Temba alisema kuwa lazima uongozi wa shule na jamii kuweza kuweka utaratibu wa kuwalinda watoto hao wa kike kupata elimu badala ya kuwafukuza shule baada ya mimba na kuwa kilichofanywa na uongozi wa shule hiyo ni hakiungwi mkono na wanaharakati hao .

Huku Gaso akisema kwa kuwa zipo tetesi kuwa mtuhumiwa wa mimba hiyo amehonga kiasi cha shilingi milioni 1 kwa uongozi wa shule ,mzazi na serikali ya mtaa ili kuficha suala hilo ni vema TAKUKURU kufuatilia suala hilo zaidi .

Kaimu afisa elimu wa shule za msingi Manispaa ya Iringa Vicent Kalinga alisema kuwa uongozi wa shule hiyo hauna uwezo wa kumfuta mwanafunzi shule bila kuwepo na maamuzi ya kamati ya shule na kuwa iwapo uongozi wa shule umemfuta shule mwanafunzi huyo bila baraka za kamati ya shule ni kosa kubwa ambalo litapelekea wahusika kuchukuliwa hatua kali ila kama ipo Mihtasari inayoagiza mwanafunzi kufutwa shule kutoka kamati ya shule ndio itakuwa ni pona kwa mkuu wa shule hiyo.
Habari kwa hisani ya Francis Godwin 

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa