:
Mwanafunzi Honolina Msigala aliyefutwa kuendelea na masomo ya elimu ya Msingi baada ya kupata mimba ,kulia ni baba mzazi mzee Msigala na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Isakalilo kulia
Mkuu wa shule ya Msingi Njiapanda Patrick Mayemba(kushoto) baba wa mwanafunzi aliyefutwa Honolina Msigala mzee Msigala na afisa wa kituo cha msaada wa sheria wanawake na watoto mkoa wa Iringa Bw Jackson Gaso wakiwa darasa la saba ambalo mwanafunzi Honolona alipaswa kuwepo na wenzake
MWANAFUNZI Honolina Msigala (15) mkazi wa Isakalilo katika Manispaa ya Iringa aliyekuwa akisoma katika shule ya Msingi Njiapanda katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa amefutwa katika orodha ya wanafunzi wa darasa la saba wanaosubiri kufanya mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya Msingi baada ya kudanganywa kwa Chipsi na soda ya kujazwa mimba na dereva wa lori mjini Iringa Ndanga Kilovele.
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umebaini kuwa mwanafunzi huyo amefutwa katika orodha ya wanafunzi hao wa darasa la saba ambao wanatakiwa kufanya mtihani huo wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka huu baada ya kuonekana na mimba na jitihada za mhusika wa mimba hiyo kutaka kuitoa kushindikana.
Mbali ya mwanafunzi huyo kufutwa katika orodha hiyo ya watakaofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi pia uongozi wa shule hiyo ya Msingi Njiapanda umelifuta jina la mwanafunzi huyo katika orodha ya wanafunzi wa shule hiyo kama njia ya kuficha aibu hiyo ya mimba shuleni hapo.
Baba mzazi wa mwanafunzi huyo Auzebio Msigala alisema kuwa kutokana na mtoto wake kufukuzwa shuleni kwa madai ya kupata mimba kuwa alifika katika shule hiyo na kukutana na walimu ambao walidai kuwa wamempima mtoto huyo na kumkuta na mimba na hivyo kulazimika kumfukuza shuleni hapo .
Msigala alisema kuwa mtoto huyo alikuwa akiishi na mama yake mzazi ambayo alikuwa akimtumikisha katika shughuli za kuuza pombe jambo ambalo lilimwezesha kijana huyo kutumia mwanya huo kumrubuni mwanafunzi huyo na kuanza mahusiano ya kimapenzi hadi kumjaza mimba.
"Mimi na huyo mama wa mtoto tumetengana kwa muda mrefu zaidi ya miaka mitatu sasa na mama ndie alikuwa akiishi na mtoto huyo japo malezi yake hayakuwa mazuri kutokana na mtoto huyo kumtumikisha kazi hatari za kuuza pombe huku yeye na mtoto kila mmoja akilala nyumba tofauti tofauti "alisema
Baada ya mtoto huyo kufukuzwa shule alilazimika kufuatilia suala hilo shule na kuelezwa kuwa tayari suala hilo limefikishwa katika vyombo vya dola kwa maana ya polisi na alipojaribu kufuatilia polisi alikutana na mama wa mtoto na mwanaume mwingine aliyejitambulisha kuwa ni baba wa mtoto huyo ambao walikuwa wakijaribu kufanya mazungumzo na mtuhumiwa wa mimba hiyo ili kuifuta kesi hiyo .
Alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo alifika polisi ili kuweza kusimamia jarada hilo japo mtuhumiwa baada ya kuona mambo magumu hakuweza kufika kituo cha polisi na kukimbia kabisa mji wa Iringa japo zipo taarifa kuwa mzazi mwenzake huyo na mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Njiapanda wamepokea kiasi cha shilingi milioni 1 kutoka kwa mtuhumiwa ili kujaribu kuficha suala hilo.
Msigala alisema kuwa hakubaliani na hatua ya uongozi wa shule hiyo kumfuta mtoto wake shule kwa madai kuwa ni mtoro wakati uongozi wa shule hiyo ulihusika kumpeleka Hospitali mwanafunzi huyo kupima mimba ya kutoa taarifa kwa wazazi kuwa mtoto huyo hataendelea na masomo kutokana na mimba .
Huku kwa upande wake mama wa mtoto huyo Sikujua Mkiwa alidai kuwa kwa upande wake hausiki na biashara ya kumuuza kimwili mtoto wake huyo na kuwa anachojua katika suala hilo ni dereva huyo Kilovele ambaye amehusika kumjaza mimba mtoto huyo kuwa alikuwa ni mteja katika chumba chake cha kuuza pombe ya kienyeji eneo la Isakalilo.
Akielezea mazingira yaliyopelekea kupata mimba mwanafunzi Honolina alisema kuwa kijana huyo Kilovele kuwa kwa mara ya kwanza walikutaka katika eneo hilo ambalo mama yake amekuwa akiuza pombe na ndipo alipoanza kumrubuni kwa kumwachia chenji za pombe na kumtoa kwenda bar moja iliyopo eneo la Mlandege (jina limehifadhiwa) na huku kumnunulia soda na Chipsi na kukutana kimwili kabla ya kumjaza mimba .
Alisema kuwa baada ya kijana huyo kubaini kuwa tayari ana mimba alijaribu kumpa dawa za kienyeji kwa ajili ya kuitoa mimba hiyo ilishindikana kutokana na kuwa na mimba hiyo kuwa umri wa miezi mitatu na hivyo kulazimika kukimbia na kumtelekeza katika nyumba ya kulala wageni ambako alikuwa akiishi kwa zaidi ya miezi miwili .
Bofya hapa kuendelea na habari: Francis Godwin Blog
0 comments:
Post a Comment