NA FREDY MGUNDA, IRINGA
MJUMBE
wa Halmashauri kuu CCM Taifa (NEC )Salim Abri amesema kuwa CCM Mkoa wa
Iringa itamshughulikia mtendaji yeyote wa Serikali atakayeonyesha
dalili ya kukwamisha juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya
muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
Kauli
hiyo aliitoa mwishoni mwa mwiki alipokuwa akiongea na wananchma wa CCM
Manispaa ya Iringa katika maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM
,alisema Mtu yeyote ndani ya serikali ya mkoa wa Iringa atakayeonyesha
dalili za kuhujumu au kwa makusudi, serikali ya chama cha mapinduzi
haita muacha na lazima itamshughulikia.
“Nasema
hatuta kubali kuona mtu yeyote atakaye onyesha kukwamisha juhudi wakati
rais na mwenyekiti wetu wa Taifa tutapambana nae,Rais amejitoa kwa
wananchi wake alafu mtu atokee tu na kuvuruga utaratibu lazima
haiwezekani na tutapambana nae”alisema MNEC
Alisema
Wakuu wa Wilaya wanapaswa kuwaambia viongozi wao wa serikali kuwa
kofia na nguo za kijani ndiyo wanaosimama kwenye majukwaa kuwatete
wao,hivyo si haki CCM tubebe lawama kwa ajili ya hao watendaji wazembe
wenye nia ovu kwa serikali ya kukwamisha maendeleo ili wengine wapande
jukwaani wakitukane chama Tawala.
hivyo
aliwataka viongozi wa chama hicho kujua majukumu yao ya kuhakikisha
CCM inasimammia Serikali na si wengine wanasimama kutetea uozo wa
watendaji hao ambao nia yako ni mbaya lakini kama watendaji wangejua
thamani ya CCM basi ingekuwa vigumu kuwepo mtendaji wa serikali ambae
ni mpinzani.
Abri
( ASAS ) aliongeza kuwa Ilani inataka yaale mambo yaliyaidiwa kwa
wananchi yanatekelezwa kwakuwa wakati wa kuomba kura ni wanaCCM ndiyo
waliosimama kuomba kura na si taasisi za serikali au Mkurugenzi wa
Halmashauri,hivyo hatuna budi kuhakikisha Ciongozi wa CCM wanafuatilia
utekelezaji wa Ilani kwani hata pale yasipotekelezwa wananchi halaumu
chama tawala na si watendaji wa serikali.
“Sisi
viongozi wa mkoa hapa wa CCM ndiyo wawakilishi wa mwenyekiti wetu na
madhumuni ya ccm ni kuisimamia serikali ,haiwezekani CCM tunatukanwa
ovyo kwa ajili ya wazembe,wakati serikali inasema hakuna michango
mashuleni lakini mwalimu mwenye itikadi ya kipinzani anafukuza
mwanafunzi eti bila michango hakuna kuingia”.
Alisema
MNEC “Haiwezekani Rais afanye kila juhudi alafu watokee watu wengine
wajinga tu hivi waanze kukamisha ,sisi hapa wajumbe wa Halmashauri
kuu,mwenyeviti na na viongozi wengine ndani ya chama kazi yetu nini,
yaani rais atoke ikulu aje Iringa kushughulikia watu hao ”.
Aliongeza
kwakusema “haiwezekani wananchi maskini watekeseke kwa ajili ya
wapuuzi puuzi wajanja ,rais kila siku anapiga kelele muwe kwenyenupande
wa wanyonge au upande wa maskini ,lakini kuna watu ambao kazi yao ni
kikwamisha juhudi na kubeza kazi inayofanya Rais Magufuli tunasema
hatuta kubali “
Au
mtu yeyote wa serikali atakaye taka kukwamisha juhudi za Rais na
Mwenyekiti wetu wa Taifa lazima tutamshughulikia na wanaCCM
wawashughulikie kwa sababu wanaotukwanwa ni chama cha mapinduzi na ni
kwa ajili ya uzembe wa watendaji wa serikali wasiokipenda chama
“Kwa
sababu CCM ndiyo chama kilichopo madarakani na hata kwenye kuomba kura
wao hawakuwepo lakini Mkurugenzi au mwandisi amepewa fedha ya
kutengeneza barabara alafu akala hela nawauliza lawama itaenda kwa nani
kwa kawaida itaenda kwa chama tawala ambacho ndiyo CCM basi na sisi
tusikubali”alisema,
Pia
aliwataka wanaCCM wa mkoa wa Iringa kuwapuuza wale watendaji wa
serikali wanaosema hali ngumu kwani hao ndiyo watumishi waliozoea kula
rushwa,mafisadi na watendaji wasiokuwa na maadili ya kazi.
“Alafu
wapuuzeni wale na watumishi wa serikali na viongozi wanaokasikiri na
kulalamika kuwa hali ngumu,vyuma vimaekaza sasa mimi namuuliza mshahala
wako huupati anaupata katika tarehe zilezile na je mshahara umepunguzwa
hapana ni uleule sasa ugumu unatoka wapi ,nikagundua kuwa hao ndiyo
wanaotupa tabu serikalini”alisema Abri .
Aidha
amewashukuru wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Iringa wa CCM kwa
kuwafuta machozi wanaManispaa ya Iringa ,hawa wamekuwa mstali wa mbele
katika kusukuma gurudumu la maendeleo katika Manispaa hii lakini si kama
wahawajali wa mufindi,kilolo wa Iringa Vijijini ni kutokana majimbo hao
kuwa na wabunge wa ccm lakini Manispaa ni yatima.
“Katika
miaka miwili na nusu Manispaa ya Iringa imeonza zahama kubwa kwani
hakukuwa na lolote lililofanyika katika jimbo hili zaidi ya maneno
tu”alisema
Alisema
anashangazwa na Ofisi ya Meya ambayo ni ya serikali kugeuzwa ndiyo
ofisi ya kutolea matamko ya chama chao “kila mara inawaita waandishi
wa habari kutoa matamko ya kisiasa ya chama chao na si kuwaita kuwaeleza
wamefanya nini lakini katika Manispaa ya Iringa lakini hutaona CCM
inatumis majengo ya Serikali kutolea matamako kwa sababu CCM inaofisi
zao”.
Pia
MNEC aliwata WanaCCM wa Manispaa ya Iringa kuhakikisha hawafanyi makosa
kama waliofanya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 inatakiwa waseme
sasa basi.
“unajua
kweli wanasiasa tunacheza siasa lakini tusicheze kwenye maisha ya watu
sanjali na hali za watu ,tusiweke utani wa siasa kwenye maisha ya watu
kwani siasa si kama ushabiki wa mpira,tunajenga maisha ya watu ,manispaa
yetu inakuwa kila kukicha kwa kuwa watuwanaongezeka”alisema MNEC .
Awali
akimkaribisha Mgeni RAsmi ambaye ni MNEC wa Iringa ,Katibu wa CCM Mkoa
wa Iringa Christopher Magalla aliwata aliwata watendaji wa serikali na
taasisi zake kuwa watekerezaji wa sera na maamuzi ya chama tawala kwani
ndiyo chama kilichochaguliwa na wananchi.
Kwa
hiyo asitokee mtendaji yeyote wa serikali au kiongozi anayetaka
kukwamisha sera na maamuzi ya CCM bali wawe mstali wa mbele katika
kutatua kero za watu na si wao kuwa sehemu ya kero kwa wananchi wao
wanaowategemea .
Magalla
alisema watendaji hao wanatakiwa kuhakikisha wanangaile na shida za
wananchi kwani hivi sasa kumekuwa viongozi wa serikali ndiyo wamekuwa
kero kwa wananchi kwa kuwasumbuasumbua mara kwa mara bila hata kuwapa
elimu kwanza wananchi kabla ya kuwavunjia au kukamata vifaa vyao
aambavyo ndiyo vinawaingizia kipato.
0 comments:
Post a Comment