Home » » NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, MHE. JAPHET HASUNGA AKABIDHI MSAADA WA MABATI KWA SHULE YA MSINGI ILIYOATHIRIKA NA KIMBUNGA MKOANI IRINGA

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, MHE. JAPHET HASUNGA AKABIDHI MSAADA WA MABATI KWA SHULE YA MSINGI ILIYOATHIRIKA NA KIMBUNGA MKOANI IRINGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakitwanga Kinu wakati wa ziara yake katika Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) jana Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kijiji cha Ubwachana, Donatus Lihoha mabati 60 kwa ajili ya kuezeka vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Kipanga ambayo iliezuliwa na kimbunga hivi karibuni ikiwa ni kutambua mchango wa wananchi katika uhifadhi shirikishi wa Kituo cha Mali Kale cha Isimila jana Mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akimsikiliza Mhadhiri wa Chuo Kikuu Iringa, Jimson Sanga ambaye pia ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa Fahari Yetu unaojishughulisha na Uhuishaji, Uendelezaji na Utangazaji wa utalii Nyanda za Juu Kusini kuhusu Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) wakati wa ziara yake jana Mkoani humo. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale wa Wizara hiyo Digna Tillya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Mhadhiri wa Chuo Kikuu Iringa, Jimson Sanga ambaye pia ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa Fahari Yetu unaojishughulisha na Uhuishaji, Uendelezaji na Utangazaji wa utalii Nyanda za Juu Kusini wakati akitoa maelezo kuhusu Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) wakati wa ziara yake jana Mkoani humo. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kulia kwake).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na watumishi wa Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) alipotembelea Makumbusho hiyo jana wilayani Iringa.
Na Hamza Temba - WMU

Katika jiihada za Serikali za kuendeleza ushirikiano na jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa msaada wa mabati sitini kwa ajili ya kuezeka madarasa ya shule ya msingi Kipanga baada ya kuezuliwa na kimbunga hivi karibuni katika kijiji cha Ubwachana Wilaya ya Iringa mkoani Iringa.

Msaada huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga alipotembelea kituo cha Malikale cha Isimila mkoani humo ambacho kinapakana na shule hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja Mkoani humo.

Akikabidhi mabati hayo, Naibu Waziri Hasunga alisema Serikali inatambua mchango wa wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi kwenye uhifadhi shirikishi hivyo ni jukumu la Serikali kuwaunga mkono pale wanapopatwa na majanga ya aina mbalimbali.

Aidha, aliwataka baadhi ya wananchi wanaochimba mchanga kwenye maeneo ya vivutio katika kituo hicho waache mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwakuwa wanahatarisha uhai wa kingo za miamba ya kale ambayo na kivutio kikubwa cha utalii wa asili katika ukanda wa kusini.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa