Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) Mkakati wa Dkt.
Kissui Stephen Kissui akielezea malengo ya ziara YA Wakulima wanachama
wa mtandao huo walipowasili katika eneo la shamba hilo lililopo Ruaha-
Kware, wilayani Kilolo, mkoani Iringa, patakapolimwa zao la kibiashara
la Papai. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa mtandao
huo, Adam Ngamange, Wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Kilimo na Mifugo
wa Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, John Mchopa, na Mwenyeji wa Shamba
hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.
Dk. Kissui amesema lengo ya ziara hiyo ni kuwaonesha Wakulima wanachama
wa Mkikita mashamba wanayotarajia kuanza kulima kwa mkataba pia
kuutangaza mtandao huo ili watu waanze kuwaza kijani na kila mtu arudi
kwenye kilimo.
Alisema
kama mtu hawezi kulima mwenyewe kuna wataalamu mbao watawekwa shambani
kwa gharama nafuu ambao wataweza kuendeza mashamba hayo.
Pia,
Dk. Kissui alisema wanatumia mbegu za kisasa zinazozalisha mara tatu
zaidi na mbolea za Organic ambazo hazina madawa na haziharibu ardhi ili
kuhakikisha vizazi na vizazi viweze kufurahia. Alisema pia Mkikita
husaidia kutafuta masuala ya masoko duniani kabla ya kuanza kulima zao
husika.
"Sisi tunaanza kutafuta masoko ya ndani na nje na baadaye tunawaaunganisha wakulima kwenye masoko" Alisema Kissui.
Wanachama
wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) wakiwasili Ruaha -Kware
Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa wakati wa ziara ya kujionea shamba
lenye ekari 3000 kwa ajili ya kuwekeza Kilimo cha PAPAI.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akielezea miradi ya kuhamasisha
kilimo na ufugaji kibiashara wakati wa ziara ya kutembela shamba kwa
ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa
Iringa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Mtandao wa Kijani
Kibichi Tanzania, Adam Ngamange alisema katika mtandao wanafanya miradi
ya uhamasishaji kilimo na ufugaji kibiashara.
Alisema
waligundua Watanzania wengi wanalima lakini si kibishara ambapo
wameanza na miradi mitano katika maeneo maalum kama Ruaha ambako
waendesha kilimo cha Papai kwa kufuata taratibu zote za msingi za kilimo
hai.
Aliongeza
kuwa mradi huo utakaoanza na ekari 384 zitakazogawanywa katika mafungu
ya ekari 32 na kupandwa katika utaratibu wa kili mwezi mara moja ili
waweze kusambaza papai kwenye masoko makubwa.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakitembelea na kukagua shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui (katikati) amueleza jambo Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.
Mwenyeji
wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha (alienyosha mkono), Amani Matinya
akiwaonesha wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania ukumbwa
shamba hilo na mbinu zinazotumika kumwagilia.
Muonekano wa shamba hilo.
Wanachama
wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakielekea kujionea maji
yanayotoka Mto Lukosi unaotumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Wanachama
wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakiangalia mashine zinazovuta
maji kutoka Mto Lukosi kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Muonekano wa Mto Lukosi.
Mmoja
wa wakulima wa eneo la Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa
(kulia) akifafanua jinsi maji yanavyo sambazwa kwa wakulima.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo.
Wanachama
wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakipanda kwenye basi tayari
kuanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam. HABARI/ PICHA NA KAMANDA WA
MATUKIO BLOG
0 comments:
Post a Comment