Home » » MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA

MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mwenyekiti chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamuakizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

 Na Fredy Mgunda,Mufindi

Chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimemuomba mkurugenzi kuwakopesha viwanja walimu ili kujikwamuamua na mazingira magumu wanayokumbana katika nyumba wanazoishi.

Hayo yalisemwa na mwenyekiti chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale alisema kuwa walimu wamekuwa wakiishi katika nyumba chakavu au mbali na mazingira ya shule kitu kinachosababisha kushuka kwa uwezo wa walimu kufundisha.

Kimbale alisema kuwa walimu hawana pesa za kununua moja kwa moja viwanja hivyo kwa njia ya kuwakopesha inawezekana kutokana kuwa ni waajiliwa wa serikali na mishahara yao inajulikana na ni rahisi kuresha mkopo huo.

“Sisi walimu ukitaka kujua mimi nalipwa shilingi ngapi ni rahisi tu kwa kuwa mishahara ya serikali mara nyingi inajulikana hasa pale mtumishi unapoenda kukopa mahali ndio maana tunaiomba serikali itusaidie kukopa viwanja kuwa kuwa tunauwezo wa kulipa kwa awamu tatu” alisema Kimbale
Aidha Kimbale aliwatupia lawama maafisa elimu na walimu wakuu wa shule kwa kuwanyima ruhusa bila kuwa na sababu maalum. 

“Wakurugenzi amekuwa ametoa kibali upewe ruhusa lakini viongozi waliochini ya mkurugenzi wanatuwekea vipingamizi ambavyo havieleweki kitu kinachozua utata mkubwa baina ya viongozi na walimu ambao sio viongozi” alisema Kimbale

Kimbale alimpongeza wakurugenzi wa halmashauri ya mufindi na mji wa mafinga kwa kuwajali walimu kwa kuwapa ruhusa pale inapotakiwa tofauti na hali ilivyo kwa hawa viongozi wa chini yake.

“Unakuta siku ya wanawake duniani au siku ya walimu duniani bado walimu wananyimwa ruhusa wakati muda huo mkurugenzi amewaruhusu walimu kuhudhuria sherehe hizo kitu kinachoongeza ukakasi baina ya watendaji wa nafasi za juu na watendaji wa nafasi za chini” alisema Kimbale


Kimbale aliwapongeza walimu wa manispaa ya Iringa kwa kuendelea kufanya kazi kwa kujituma licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali ikiwepo kunyimwa ruhusa.

Akijibu hoja hizo mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamu alisema haelewi kwanini mara kwa mara swala hilo linakuwa linajirudia maana tulishalitafutia ufumbuzi hapo awali.

Sasa naenda kuandika barua rasmi kwa wakurugenzi ili kutatua kabisa tatizo hilo maana hata kwangu imekuwa kero na mwazoni nilijua wakuu wa shule ndio tatizo kumbe maafisa elimu ndio tatizo naenda kulishughulikia kwa haraka sana swala hili” alisema Williamu

Williamu aliwataka maafisa elimu na wakuu wa shule wote wa wilaya ya Iringa kuwapa ruhusa walimu pale ambapo wanapata matatizo maana hakuna haja ya kumnyima ruhusa mtu akiwa anashida na watakiwa kuzifahamu siku za kitaifa ambazo ni lazima walimu wahudhurie wanapaswa kutoa ruhusa bila kipingamizi.

“Kunasiku kama siku ya mwalimu,siku ya wanawake na siku nyingine za kitaifa walimu wanapaswa kupewa ruhusa kwenda kuhudhuria tukio hilo kutokana na umuhimu wake” alisema Williamu

Williamu alisema kuwa mkurugenzi ndio mwajili sasa hao maafisa elimu na wakuu wa shule wanatoa wapi hiyo jeuri ya kuwanyima ruhusa ambayo viongozi wa ngazi za juu wanajua kuwa kunakitu kinafanyika cha taifa.

Williamu aliwataka viongozi wa walimu kuandika barua ya kuomba viwanja ili waweze kulishughulikia swala hilo likiwa kwenye maandishi.

“Andikeni barua yenye idadi na majina ya walimu wanaotaka viwanja ili kuondoa kasumba ya kusema wanaotaka ni kikukindi cha walimu wachache tu na bila kufanya hivyo swala lenu la kuomba viwanja litakuwa gumu kulitafutia ufumbuzi” alisema Williamu
Williamu aliwaomba walimu wawewavumilivu katika kipindi wacholishughulikia swala hilo kwa kuwa sio jambo la kukurupuka linahitaji utulivu wa kutosha ili kufanikishwa swala walimu kupata viwanja.

Naye afisa elimu wa wilaya ya Mufindi alisema kuwa watawatafuta hao maafisa ambao wanawanyima ruhusa walimu wakati swala hilo lilishatafutiwa ufumbuzi.

“Jamani sisi huku sheria tulishaiweka kwenye matukio muhimu ya kitaifa walimu wapewe ruhusa sasa sijui ili sawala limetoka wapi naomba nikitoka hapa nitazungumza na wakuu wa shule pamoja na maafisa elimu wenzangu”


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa