Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge
wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati akiwa katika moja ya shule ya msingi akiwa katika ziara ya
kutambua changamoto na kuzifanyia kazi ili ziwe na ubora kama shule za
watu binafsi na kuongeza ufaulo kwa wanafunzi wanasoma katika shule
hizo.
Mbunge
wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati akiwa darasani na wanafunzi wa shule ya msingi Kibwabwa iliyopo
kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa
Mbunge
wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati akiwa na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya
kuzitambua changamoto za shule za msingi.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge
wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati amefanya ziara kwenye baadhi ya shule za msingi za manispaa ya
Iringa kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo na kuanza kuzitafutia
ufumbuzi kwa lengo la kuboresha mazingira ya wanafunzi kusomea.
Akizungumza
mara baada ya kumaliza zira hiyo ya wiki moja Kabati alisema kuwa
amefanya ziara katika shule ya msingi Kihesa,Igereke,Mtwira na shule ya
Kibwabwa na kubaini changamoto nyingi ambazo anaanza kuzitafutia
ufumbuzi hivi karibuni.
“Nimejionea
mwenyewe changamoto zilizopo na naona kama changamoto kwa asilimia
kubwa zinafanana hivyo ni kazi yangu kuanza kutafuta njia ya kuanza
kuzitatua changamoto hizo”alisema Kabati
Kabati
alisema kuwa atakikisha anazikarabati shule hizo kwa kushirikiana na
wadau wa maendeleo kama nilivyofanya hapo awali katika shule za msingi
za Azimio na Kigonzile ambazo kwa sasa zinaubora kama shule za watu
binafsi.“Kwa kweli wadau wamekuwa wakinisaidia kufanikisha
swala la kukarabati shule za msingi zilizopo hapa manispaa ya Iringa
ili kuhakikisha mazingira ya shule zote yanakuwa bora kama shule za watu
binafsi” alisema kabati
Aidha
Kabati aliwataka viongozi wa serikali na viongozi wa kisiasa
kuzitembelea shule hizo mara kwa mara ili kutatua matatizo haya mapema
kwa sababu shule nyingi ni kongwe ndio maana miundombinu imeharibika kwa
kiasi kikubwa.
“Viongozi
wengi tunashinda sana maofisini kuliko kwenda kuyatembelea maeneo yenye
changamoto kama hizi za shule za msingi za manispaa ya Iringa kwasababu
ukitembelea maeneo yenye changamoto mara kwa mara inakuwa kazi rahisi
kuzitafutia ufumbuzi mapema” alisema Kabati
Kabati
alisema kuwa shule nyingi za msingi manispaa ya Iringa zilijengwa miaka
1980 ndio maana saizi miundombinu imeharibika kutokana na
kutokarabatiwa mara kwa mara na kusababisha kuendelea kuharibika kwa
kuwa hakuna mikakati ya makusudi ya kukarabati shule hizo.
Kabati
aliwaomba wananchi na wadau wa maendeleo kutoa ushirikiano wa kutosha
ilikufanikisha azma ya kuzikarabati shule hizo na kuacha kuangalia
Itikadi ya vyama vya siasa kwa kuwa maendeleo hayana siasa.Naye
mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Kibwabwa Isumael Mlenga
alimpongeza mbunge huyo kwa kazi anayoifanya ya kusaidia kukarabati
shule za msingi za manispaa ya Iringa ni jukumu kubwa analolifanya kwa
wanairinga.
“Ni
wabunge wachache wenye moyo kama wa Ritta Kabati hivyo tunapaswa
kuendelea kumuunga mkono kwenye kazi anazozifanya kwa maendeleo ya
watoto wetu wanaosoma katika shule hizo zinazokarabatiwa na mbunge huyo”
alisema Mlenga
Karumerita
Mbuta,Zubeiry Mlowela na Romana Lutenga ni wajumbe wa kamati ya shule
ya Kibwabwa walimpongeza mbunge huyo kwa ziara zake anazozifanya
kuzitambua Changamoto zilizopo mashuleni hasa kwenye shule za msingi
hivyo tunaomba ziara zako ziwe na matunda kwa kuboresha miundombinu ya
shule ulizotembelea.
Kwa
upande wake mkuu wa shule ya msingi Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti
wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru mbunge Ritta Kabati
kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi
katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.
0 comments:
Post a Comment