Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza wakati wa mkutano wa
utambuzi wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga wilayani
mufindi mkoani Iringa
Prof
Aldo Lupala akitambulisha na kuelezea jinsi gani walifanikiwa kuundaa
mpango huu kwa tija na maendeleo ya halmashauri ya mji wa mafinga
Mwenyekiti
wa halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga akiwa na mkuu wa mkoa
wa Iringa Amina Masenza sambamba na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri
williamu wakati mkutano wa utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri
ya mji wa mafinga
Na Fredy Mgunda,Iringa
Halmashauri
ya mji wa mafinga wilayani mufindi mkoani Iringa yajipanga kuwa
manispaa kwa kuanza kuupanga mji kuwa wa kisasa na wakibiashara kwa
kutumia wataalamu kutoka chuo cha SUA na wataalamu kutoka halmashauri
hivyo.
Akizungumza
wakati wa kikao cha mpango kabambe wa mji wa mafinga mkuu wa mkoa wa
Iringa Amina Masenza alisema kuwa mji wa mafinga unatakiwa kukuwa kwa
mpangilio unao stahili hivyo kuanza na mpango huu itakuwa njia mbadala
ya kutatua changamoto mbalimbali za miundo mbinu ambazpo mikoa mingine
kuna migogoro mingi.
“Niwashukuru
wataalamu na viongozi wa halmashauri hii kwa kazi kubwa mliyoifanya ya
kubuni na kuanzisha mpango kabambe ambao utakuwa mfano kwa halmashauri
nyingine zinazokuwa kwa kasi na hazina mpango kama huu” alisema
Masenza
Masenza
aliwataka viongozi na wadau wa maendeleo katika halmashauri hiyo kutoa
elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya mpango huo kabambe ambao utasaidia
kukuza mji kwa kasi na kuwa na mpangilio unaotakiwa hapa nchi.
“Sasa
naona tuliopo hapa tunatosha kufikisha ujumbe huu kwa wananchi na wadau
wengine ambao hawajahudhuria mkutano huu ili jamii kuwa na elimu na
kuondoa migogoro na minong’ono iliyopo kwa wananchiwasiojua chochote
kuhusu mpango huu” alisema Masenza
Aidha
masenza aliwashukuru wataalamu kutoka chuo SUA kwa kufanikisha mpango
kabambe huo kwa gharama nafuu tofauti wangepewa makampuni binafsi ambao
mara nyingi gharama zao huwa juu sana tofauti na taasisi za kiserikali
na kuitaka halmashauri ya mji wa mafinga kuendelea kuzitumia taasisi za
kiserikali zenye uwezo na vigezo stahili kweli miradi mbalimbali ya mji
wa mafinga.
Kwa
upande wake mwenyekiti ya halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga
alisema kuwa mpango kabambe huu utadumu kwa takribani miaka hamsini
ijayo hivyo wakazi wa halmashauri hiyo watanufaika kwa kuwa na mji ambao
utakuwa umepangiliwa kwa kila kitu.
“Mkuu
wa mkoa nikuahidi kuwa mpango huu utakuwa wa miaka mingi na tutafuata
mambo mazuri yote kutoka kwa wataalamu ili kuufanya mji wa mafinga kuwa
kivutio cha miji mingine na kuwafanya watu wenngine kuiga mfano kutoka
kwetu” alisema Makoga
Makoga
aliwapongeza wanafunzi, wataalamu wa chuo cha SUA pamoja na wataalamu
kutoka halmashauri kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya kuhakikisha
mpango huo kukamilika kwa wakati pasipo kuwa na changamoto zozote zile.
Halmshauri
ya mji wa mafinga tunategemea hivi karibuni kuwa manispaa kwa kuwa
vigezo karibia vyote tunavyo hivyo tunaomba kuendelea kushirikiana na
kushauriwa katika mikakati ya kuukuza mji huu unakabiliwa na ongezeko la
watu kila siku alisema Makoga.
Naye
prof. Aldo Lupala alisema kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na wataalamu
wengi hivyo ni vyema wakatumiwa katika miradi mingi ya kimaendeleo ili
kungeza ajira na kukuza ujuzi wao pindi wawapo kazini.
“Unajua
ukiwa mtaalamu halafu huna kazi kwa kiasi fulani utaalamu au ujuzi wake
utapungua toafuti kila wakati mtaalamu akiwa kazini huongeza ubunifu na
kukuza utaalamu wake hivyo mgeni rasmi naomba tufikishie ujumbe huu
serikali kuu” alisema Lupala
Prof
Lupala aliupongeza uongozi wa halmauri ya mji wa mafinga kwa kufanya
kazi na wataalamu kutoka chuo kikuu cha SUA kwa ushirikiano mkubwa ambao
umefanikisha kupata mpango kabambe ambao utaisaidia halmashauri kwenye
mipango ya kuukuza miji huo wa mafinga kuwa manispaa.
0 comments:
Post a Comment