Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na wakazi wa
kijiji cha Ufyemba kata ya Wasa wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa katika
jitihda za kuhamasisha ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick
Golwike akihamasisha wananchi kuendeleza ari ya kushiriki kazi za maendeleo ya
kijiji chao cha Ufyemba mkoani Iringa kwa kushirikiujenzia wa zahanati hiyo ambayo unajengwa na wananchi wa
kijiji hicho kwa kutumia nguvu za wananchi wenyewe ili kusogeza huduma za afaya
kijijini.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinda akishirikiana na wakazi wa Kijiji
cha ufyemba kubeba matofali katika kufanikisha ujenzi wa Zahanati kijiji cha
Ufyemba kata ay wasa, iliyoko wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa.
Wananchi wa kijiji cha Ufyemba wakishiriki
katika kubeba matofali na kujenga jingo la zahanati ya kijiji hicho ili kuondokana
na taatizo la kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi mifuko 50 ya saruji
kwa Mwenyekiti wa Kijij cha Ufyemba Bw Ronaganius Lunyungu ili kuunga mkono
jitihada za wananchi hao katika kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha
Ufyemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akikabidhi pesa kwa Mwenyekiti
wa Kijij cha Ufyemba Bw Roganius Lunyungu zilizopatikana katika harambee ili isaidie katika kumalizia Ujenzi wa
zahanati ya kijiji cha Ufyemba.
Na Erasto Chin’goro-WAMJW
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Bibi Sihaba
Nkinga amewahamasisha wananchi kujitolea katika kutekeleza shughuliza maendeleo
ikiwa ni sehemu ya kuhamsha ari wananchi kufanya kazi za maendeleo yao.
Ameyasema
hayo katika ziara yake Mkoani Iringa wakati katika jitihada zake za kuhakakisha
jamii inahuisha ari ya kushiriki shughuli za kujitolea na uanzishaji wa miradi
inayoibuliwa na kutekelezwa na wananachi wenyewe kwa kushiriki kazi mbalimbali
za utekelezaji wa shughuli hizo katika maeneo ya mijini na vijijini.
“Dhana
ya maendeleo ya jamii inawataka wananachi kujitolea kushiriki kazi za maendeleo
kwa kushirikisha kubaini mahitaji na changamoto zinazowakabaili wananachi na
kujadiliana pamoja kuhusu mbinu za utatauzi wa changamoto hizo” alisema Bibi
Sihaba.
Bibi
Sihaba ameongeza kuwa wananchi waendelee kuainisha ushiriki wao katika
kukamilisha miradi hiyo ya pamoja kwa kutumia rasilimali na nguzu kazi ya ndani
badala ya kutegemea misaada ya nje ya jamii.
Aidha Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wananchi katika maeneo mengine kuiga mfano bora wa kijiji cha Ufyemba ili kujiletea maendeleo bila kusubiria msaada wa Serikali kuu.
Dhana
hii ya kujitolea katika kutekeleza shughuli za maendeleo imefanikisha kijiji cha Ufyemba kata ya Wasa kilichoko
wilaya ya Iringa vijijini, mkoani Iringa kushirikiana na wananchi kukamilisha
ujenzi wa zahanati ili kupata uhakika wa huduma za afya kwa watoto, wanawake,
na jamii kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment