Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa
iringa wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la chanzo cha
mradi huu wa maji katika mji mdogo waIlula
Mkuu
wa mkoa wa iringa Amina masenza akifurahia kufika kwenye chanzo cha
maji pamoja na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kwa kuwa wanajua
hilo ndio litakuwa suluhisho la mda mrefu kwa wakazi wa mji mdogo wa
Ilula
viongozi
wa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa wakiwa wanaelekea kwenye chanzo
cha maji kwa ajili ya kujua jinsi gani kitaweza kutatua kero za wananchi
wa mji wa mafinga
mjumbewa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa ndugu mosha akiwa njiani kuelekea kukikagua chanzo hicho cha maji
katibu
msaidizi wa chama cha mapinduzi mkoani iringa akiwa sambasamba na mkuu
wa wilaya ya kilolo Asia Abdalla wakielekea kukagua chanzo kipya cha
maji kwa ajili ya wananchi wa mji mdogo wa mafinga
Na Fredy Mgunda,Iringa
Halmashauri
ya wilaya ya kilolo inatarajia kutatua kero ya maji iliyodumu kwa miaka
mingi katika mji mdogo wa Ilula mkoani Iringa kwa kutenga kiasi cha
dola za kimarekani 9,548,827 kwa ajili ya kujenga chanzo kipya cha maji
yatakayo weza kutatua changamoto hiyo.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kukagua utekeleza wa ilani ya chama cha mapinduzi
wilayani kilolo mkuu wa mkoa wa iringa ambaye ndio mwenyekiti wa kamati
ya siasa ya mkoa bi Amina Masenza alisema kuwa wameamua kutafuta chanzo
kipya ili kutatua tatizo la maji katika mji mdogo wa Ilula.
“Leo
nimefika hadi huku kwenye chanzo cha maji ambacho naamini kuwa
kitafanikiwa kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi wa mji mdogo wa
Ilula hivyo lazima waisimamie ipasavyo ilani ya chama na kuhakikisha
kuwa wanatatua matatizo ya wananchi”alisema Masenza
Aidha
Masenza alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono rais
wa jamhuri ya muuungano wa Tanzania dr John Pombe Maguli kwa kazi kubwa
anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wake.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alivitaja baadhi ya
vyanzo ya maji na uwezo wa uzalishaji ambavyo vinatoa huduma kwa mji
mdogo wa Ilula ni Ilomba kutoka kijiji cha Imalutwa na Idemule kutoka
kijiji cha Mazombe kwa ujumla vinazalisha wastani wa uzalishaji wa maji
wa mita za ujazo 1,142 kwa siku.
Abdallah
alisema kuwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula unamahitaji makubwa ya
matumizi ya maji ambapo kwa siku wanahitaji maji ya mita za ujazo 2687
kwa siku hivyo hadi sasa kunaupungufu wa mita za ujazo 1545 kwa siku.
“Mji
huu unakuwa kwa kasi kubwa hivyo matumizi ya maji yamekuwa makubwa mno
ndio maana tumeanza kujenga chanzo kingine ambacho kitakuwa na
suluhisho kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula na kutaua kabisa tatizo la
maji” alisema Abdallah
Abdallah
aliwataka wananchi na viongozi wa ngazi zote kuacha tabia ya kuharibu
vyazo vya maji na mazingira kwa ujumla hivyo atakaye kamatwa anafanya
uhalibifu wowote ule sheria itachukua mkondo wake.
“Ni
malufuku kwa wakulima kulima kwenye vyanzo vya maji,wafugaji kufujia
mifugo kwenye vyanzo vya maji pamoja na ukaji wa miti hovyo hapo
nitakuwa mkali sana kwa watu ambao watakiuka haya nayoyasema hii leo kwa
kuwa kila kitu kipo kisheria “ alisema Abdallah
Naye
meneja wa mamlaka ya maji wa mji mdogo wa Ilula Enock Ngoyinde aliiomba
serikali ya na kamati ya siasa ya mkoa wa iringa kusaidia upatikanaji
wa pesa kwa wakati za kumaliza mradi huu wa maji ili wananchi waanze
kupata huduma bora mapema iwezekanavyo.
Ngoyinde
alisema kuwa mradi huo ukikamilika utakuwa umeongeza eneo la utoaji wa
huduma vya maji kutoka wastani wa asilimia 62 hadi asilimia 75 na
kuwahudumia wananchi zaidi ya elfu ishirini na tano (25000) ambao
watakuwa na mtandao wa bomba za maji.
0 comments:
Post a Comment