Home » » Mimi natekeleza falsafa ya hapa kazi tu kwa vitendo – DC Kasesera

Mimi natekeleza falsafa ya hapa kazi tu kwa vitendo – DC Kasesera


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesera amesema katika utumishi wake kwa wananchi hana mbwembwe kama baadhi ya watu wanavyodai bali anafanya kutokana na hali halisi na eneo husika.
Kasesera ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV, ambapo ameweka wazi kwamba anafanya kazi yake ya kuwatumikia wananchi na ofisini hushinda mara chache sana ili kuonana na wananchi na kutatua kero zao katika maeneo yao.
“Mimi sina mbwembwe, mfano zile picha zinazoonyesha nikiwa kwenye maji nikiokoa watoto, kule mvua ilinyesha kitongoji kizima kikawa kinatakiwa kuokolewa ikabidi niende na viongozi wenzangu kufanya uokozi na Mungu alisaidia tukafanya vyema” Amesema Kasesera
Aidha Kasesera ameongeza kuwa baada ya kuteuliwa kwa mara ya kwanza na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete aliingia kazini moja kwa moj a hivyo hakuwahi kupata semina ya ukuu wa wilaya, na alipoteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli akawa tayari amepata uzoefu wa kuendelea kutumikia umma.
Pamoja na hayo DC Kasesera amewataka viongozi wa umma kutumia mitandao ya kijamii kwani imekuwa ikitoa taarifa mbalimbali kuhusu kero za  wananchi.
‘Mimi natumia mitandao ya kijamii mingi, hasa facebook imekuwa ikinisaidia sana ambapo watu hunitumia ujumbe mfupi ‘meseji’ na nikifuatilia mambo hayo hukuta ni kweli na kuyatatua kwa haraka.
Wakati huo huo DC Kasesera amesema hana ugomvi na viongozi wa UKAWA katika wilaya yake na anafanya nao kazi kwa ushirikiano kwani anatekeleza kwa vitendo falsafa ya ‘hapa kazi tu’.


0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa