Home » » MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Bw Venance Mwamoto amesema kuwa lengo la wananchi wa Kilolo kumchagua kuwa mbunge wao ni kutaka kuona analeta maendeleo jimboni

MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Bw Venance Mwamoto amesema kuwa lengo la wananchi wa Kilolo kumchagua kuwa mbunge wao ni kutaka kuona analeta maendeleo jimboni

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


MBUNGE  wa  jimbo la Kilolo mkoani Iringa Bw  Venance  Mwamoto amesema  kuwa lengo la  wananchi  wa Kilolo  kumchagua   kuwa mbunge wao ni kutaka kuona analeta maendeleo jimboni na  sio  kuwavunjia  heshima  wapiga  kura  wake kwa kuwa mbunge bingwa wa  kusinzia bungeni ama  kushirikia vurugu zisizo na tija .


Akizungumza leo katika  mkutano  wake  wa hadhara  katika kata ya Ng'ang'ange mkutano wa  kuwashukuru  wananchi  wa  Kilolo kwa kumchangua  kuwa mbunge  wao  kwa ajili ya kutaka  kuona wilaya  hiyo ya  kilolo  inapiga hatua katika maendeleo na  si vinginevyo .

Hivyo  alisema  kuwa mbali ya  kuwa  wapo  baadhi ya watu  wachache hasa  wapinzani  wake katika  siasa ambao wanazunguka maeneo mbali mbali ya  jimbo  hilo na  kumchafua  kuwa amefungiwa kwa  muda  wa miezi sita kushiriki  vikao  vya  bunge kwa madai ya  kuuliza  swali la kupigania  maendeleo ya  Kilolo ,alitaka  wananchi wa  Kilolo kupuuza maneno hayo kwani hakuna jambo kama  hilo na yeye hajapata  kufungiwa  wala kuonyo  bungeni .


"Naomba mtambue  huu  si  wakati wa kampeni ni  wakati wa mimi kama  mbunge  wenu  kwa kushirikiana na rais Dr John Magufuli na madiwani  kuona kazi ya  kuwaletea maendeleo  wananchi inafanyika ila  wapo  wapinzani wachache ambao  wanazunguka katika minada na  kueleza  uzushi usio na kichwa wa miguu  kuwa eti mbunge wa Kilolo amefungiwa na Rais Dr Magufuli  kushiriki  vikao  vya    bunge kwa madai  kuwa kwanini  nataka kujenga chumba cha  kuhifadhia maiti Hospitali teule ya wilaya ya  Kilolo iliyopo Ilula"

Mbunge  Mwamoto  alisema maneno hayo  yasiwakatishe nguvu wananchi wa Kilolo  kweani hakuna kitu  kama hicho na  Rais hausiki na  kumwajibisha  mbunge  wala diwani pia  hata  sipika hajapata  kumnyoshea kidole  wala kumpa onyo lolote na  kuwa  siku  zote mti unaopigwa mawe ndio  wenye matunda na yeye atazidi  kuwaletea maendeleo wananchi  wake kama alivyoanza na kuwataka  wapinzani na  wana CCM kuachana na  siasa za majukwaani  kwa   sasa ni muda wa kazi.

Hata   hivyo  mbunge  Mwamoto  alisema kuwa  lengo  lake  ni  kufanya kazi kwa moyo wote  ili  kuifanya  wilaya ya  kilolo isonge  mbele  zaidi kimaendeleo na katika  kuonyesha kwa  vitendo  kuwa  yeye si mbunge wa  kulala ni mbunge wa kazi ataomba diwani wa kata   hiyo kuandaa ukumbi wa kijiji ili alete Runinga kwa ajili ya  wananchi  wakitoka shamba  kufuatilia vikao  vya  bunge ili  kuona kama ni mbunge wa kusinzia  bungeni ama kazi.

Alisema iwapo  wananchi wake  watabahatika  kuona anasinzia bungeni pindi atakaporejea  kutoka bungeni wasisite  kumuuliza sababu ya yeye  kusinzia  bungeni.






0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa