Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
mbunge Mgimwa akitimiza ahadi yake ya bati 50 kwa kituo cha yatima Tosamaganga |
Mbunge Mgimwa katikati akitazama nguzo za umeme katika kata ya Mgama
Mbunge Mgimwa akiwa katika usafiri wa Baiskeli wakati wa ziara ya kutembelea wananchi wake kushukuru
WAKATI
wabunge wakiwa mbioni kumaliza muda wao mbunge wa jimbo la
Kalenga Bw Godfrey Mgimwa amesema kuwa kwa kipindi chake cha mwaka
mmoja kama mbunge wa jimbo hilo la Kalenga amesema anamshukuru Mungu
katika safari yake ya kuwatumikia wananchi wa jimbo la Kalenga kwa
kufanikisha kutekeleza ahadi zake kwa asilimia 99.9 ndani ya mwaka
mmoja .
Huku
akiwaomba wananchi wa jimbo hilo la Kalenga kuweza kumpima kwa
kazi alizozifanya kwa mwaka mmmoja na zile zilizofanywa na wabunge
waliotangulia katika jimbo hilo na wabunge wa upinzani kwa kipindi
cha miaka mitano walioongoza majimbo yao.
Bw
Mgimwa aliyasema haya jana wakati akieleza utekelezaji wa ilani
ya CCM na ahadi mbali mbali zilizoahidi mbunge aliyetangulia
Marehemu Dr Wiliam Mgimwa kwa kila kata kati ya kata 13 za jimbo la
Kalenga .
Alisema
kuwa katika kata ya Kiwere ahadi ambazo amezitekeleza ni pamoja na
mradi wa umeme vijiji vya Mgera ,kitapilimwa,Mfyome ambao unaendelea pia
Mradi
wa Maji, Mfyome na kiwere unaendelea,Bati 80 shule ya msingi
Kiwere,Bati 50 Itagutwa,vikundi vya vicoba kata ya kirewe vimepewa Tsh
milioni 3,ujenzi wa maabara shule ya sekondari Kiwere amechangia milioni
2 ujenzi wa bweni sekondari ya Kiwere amechangia Tsh milioni 1
kata
ya Nzihi katika shule ya Dintyus sekondari amechangia Tsh milioni
2,saruji
mifuko 100,Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara shule ya sekondari Kidamali
na mifuko 50 ya saruji, Tsh 400,000 kwa timu ya daraja la tatu ngazi ya
Mkoa wakati kata ya Ulanda Shule ya msingi Lukwambe Bati 100, ujenzi
wao kituo cha afya Mlangali mchango wa Tsh 250,000,mradi wa maji kijiji
cha Mwambao,kijiji cha Weru ,mradi wa umeme Kijiji cha Ibangamoyo
,Kibebe na Weru
Mchango wa Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara Shule ya sekondari Kalenga
Mbunge Mgimwa alisema kwa kata ya Kalenga kwa shule ya msingi amechangia Tsh 660,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo
vya wanafunzi,Bati 50 na mabelu ya nguo za yatima Tosamaganga vyote
vikiwa na thamani ya Tsh milioni 3.5 pia amechangia Tsh milioni 2
ujenzi wa maabara Sekondari ya Lipuli ,mifuko 50 ya Saruji,Vicoba kijiji
cha kalenga Tsh 500,000 pamoja na vifaa vya michezo kwa vijana
Huku kata ya Mseke katika shule ya msingi Ugwachanya Bati 60 , shule ya msingi Sadani Bati 60 na
saruji 50 na Tsh milioni 1, shule ya msingi Makota Bati 50 Mseke
sekondari Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara,kikundi cha
Sliki Tanangozi Tsh 700,000
Mradi wa umeme kijiji cha Wenda unaendelea wakati kata ya Luhota kwa upande wa Shule
ya msingi Wangama Bati 50 na saruji 50, kikundi cha siliki Tagamenda
Tsh 500,000 na Luhota sekondari Tsh milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa
maabara
Alitaja
kata nyingine ambazo amechangia kuwa ni Magulilwa kwa shule ya
msingi Nega B Bati 100,kijiji cha Mranda Bati 80, mradi wa umeme
Nega B na Magulilwa unaendelea, shule ya msingi Ng'enza Saruji mifuko
50 ,Visiwa viwili vya maji na shule ya sekondari Muwana Tsh milioni 2
ujenzi wa maabara na kata ya Lyamgungwe Kijiji
cha Malagosi Bati 80 za ujenzi wa zahanati,kijiji cha Lupembelyasenga
saruji 50 , mradi wa umeme Wenda,Kikombwe,Ismila na maji kijiji cha
Kikombwe unaendelea
Kuchangia Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara shule ya sekondari Ismila
Pia kata ya Mgama kwenye shule ya msingi Mgama Bati 100
na Tsh milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa maabara, shule ya msingi
Ibumila Bati 50 na saruji 50 ,shule ya msingi Itwaga saruji 20, shule
ya msingi Luhato madawati 30 na mradi wa umeme kijiji cha Mgama
unaendelea na kata ya Ifunda amechangia
Shule
ya msingi Mibikimitali Bati 50, Shule ya msingi Udumuka saruji
100,kijiji cha Mfukulembe Bati 50 ,shule ya sekondari Lyandembela
milioni 2 ujenzi wa maabara na Shule ya sekondari Lyasa Tsh milioni 2
Bw
Mgimwa alisema kuwa kwa kata Lumuli ,kijiji
cha Isupilo Bati Bati 50 ,kijiji cha Muwimbi Bati 80 ,Lumuli sekondari
Tsh milioni 2 ujenzi wa Maabara,mradi wa umeme Isupilo,Itengulinyi,mradi
wa maji Isupilo ,Itengulinyi na Lumuli inaendelea pia kivuko cha
barabara ya Itengulinyi - Magunga kimekamilika wakati kata ya Wasa
,Shule ya msingi Usengelendeti Bati 100,Mahanzi Bati 80,WASA sekondari
Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara,mradi
wa umeme unaendelea
Alitaja utekelezaji wa ahadi alioufanya pia kata ya Maboga katika Shule
ya msingi chamgogo Bati 50 , Shule ya msingi Kidilo bati 50, Shule ya
sekondari Kiponzero Milioni 2 ujenzi wa maabara , barabara ya Magunga -
Makota umekamilika,shule ya msingi Makombe saruji mifuko 50 pia mradi
wa umeme Kiponzero unaendelea.
Mbunge
huyo alisema kuwa jimbo la Kalenga kuna jumla ya kata 13 ila sasa ni
kata 15 ambazo zimetokana na kata mpya na kuwa kiasi cha zaidi ya Tsh
milioni 110 amepata kuzitumia kutimiza ahadi zake kwa kipindi chake
cha mwaka mmoja pekee aliopata kuwepo madakarani
Hata
hivyo alitaja ahadi ambazo bado kuzitimiza na atazitimiza wakati
wowote kabla ya kumaliza muda wake kuwa ni ahadi ya Tsh milioni 1
kwa ajili ya Vicoba Ifunda kibaoni ,bati 100 kwa ajili ya kuchangia
ujenzi shule ya wasichana Ifunda ,ahadi ya Tsh milioni 1 kwa ajili ya
ununuzi wa vyombo vya muziki katika Kanisa la Lutherani Ifunda kibaoni
na ahadi ya mwisho ni ya bati 60 kwa ajili ya shule ya sekondari
Lyandembela
Hivyo
aliwataka wananchi wa jimbo la Kalenga kuendelea kuwa na imani
zaidi kwani amefanikiwa kutimiza ahadi zilizonyingi ambazo amepata
kuzitoa kwa muda wa mwaka mmoja pekee na kuwa iwapo watamchangua
tena basi wawe na imani ya kupata maendeleo makubwa zaidi ya haya .
"
Naomba wananchi wa Kalenga niwahakikishie kuwa nitagombea tena
Ubunge kwa mwaka huu ili niweze kupata miaka yangu mitano ya
kushirikiana nanyi katika kuleta maendeleo "
|
0 comments:
Post a Comment