Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Dkt MUSA LEONARD
MDEDE akitoa neno katika kongamano la vijana wa katoliki
baadhi ya vijana wakimsikiza mdede katika kongamano hilo.
baadhi ya viongozi wa vijana hao wakiwa makini kumsikiliza mdede
mdede akiingia katika ukumbi uliokuwa unafanyika sherehe
na fredy mgunda,iringa.
Vijana kikatoliki waliokuwa
kwenye kongamano lililofanyika katika kijiji cha ulete wamewataka wananchi wa
jimbo la kalenga kuelekeza macho na masikio yao kuhakikisha wanamchagua kijana
mwenzao ambaye ameonekana kuwa na uwezo wa kuwa kiongozi bora na kuwaletea
maendeleo katika jimbo hilo.
Wakizungumza katika kongamano
hilo vijana hao walisema kuwa hawajapata kuona kijana anayejiamini na kuonesha
wazi mbinu za kulikomboa jimbo katika nyanja ya kimaendeleo.
“Jimbo la kalenga linawasomi
wengi lakini jimbo hilo bado halina maendeleo ya kuridhisha licha ya kuwa na
vitega uchumi vingi ambavyo vingeweza kuiongezea mapato na kukuza uchumi wa
jimbo hilo,kwa mipango na mbinu ambazo mose madede amezionyesha
zinatufaa kabisa wananchi wa jimbo la kalenga”. walisema vijana hao.
Lakini waliongeza kwa
kuwataka vijana na wananchi wa jimbo la kalenga
kutofanya makosa katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kumchagua kiongozi
anayewafaa na kujiamini kwa kuwaletea maendeleo na kuwatetea wananchi wake.
Nao viongozi wa vikalia tosamaganga
walimsifu kijina moses kwa kujiamina na kuwaonyenyesha vijana wenzao kwa maneno
na ujumbe wa kuwapa njia muhimu za kufikia malengo yao katika maisha.
Waliongeza kwa kusema kuwa
baadhi ya vijana waliokosa hutuba ya moses mdede wamekosa kitu
cha muhimu sana lakini akawaomba vijana hao wakirudi nyumbani kwao basi
wafikishe ujumbe kwa wananchi na vijana waliokosa kongamano hilo kwa kuwa wao
ndio mabadiliko ya sasa.
“Vijana mbadilike msiwe kama
vijana wa zamani nchi hii inahitaji viongozi wenye weledi wa kuwaongoza
wananchi na kuwalete maendeleo mdede
anafaa na anasifa zote za kuwa kiongozi kwa kuwa anasifa zote za kuwaongoza
wanachi wa jimbo la kalenga hivyo wananchi msifanye makosa”.walisema viongozi hao.
Kwa upande wake sister
kiliana sanga wa ulete alisema kuwa hajawahi kukutana na kijana mwenye
uwezo mkubwa wa kifikra na mipango madhubuti ya kuleta maendeleo ya jimbo la
kalenga.
Naye moses mdede
aliwataka vijana kujitambua na kushemu maamuzi yao wakati wananfanya kitu
sahihi kwa wakati sahihi kuwataka wasikubali kuchaguliwa kiongozi katika
uchaguzi wa mwaka huu.
“Sasa ifike wakati vijana
muwe na maamuzi ya kujichagulia viongozi sahihi vijana ni taifa la leo sio la
kesho hivyo ukimchagua kiongozi kwa kununuliwa ujue kuwa atakapo ingia
madarakani atawaongoza anavyowataka yeye na sio kuwaletea maendeleo kwa kuwa
ameingia madarakani kwa kuwanunua”.alisema mdede
mdede aliwataka vijana kuacha kulalamika kila wakati na
badala yake wafanye kazi kwa kujituma ili wajiletee maendeleo na kuacha tabia
ya kufaata mkumbo katika kutafuta maisha bora.
“Viongozi wa dini nyie mnaka mara kwa mara na waumini wenu hiyo
mnapaswa kuwapa elimu ya maisha na kuwajua viongozi wazuri kwa kuwa nyie
mnakaramu hiyo,mfano leo hii mmekaa na vijana hao na kuwapa mafunzo mbalimbali
hivyo mnapaswa kuwaambia ukweli juu ya mstakabadhi wa serikali yetu ambayo
imepoteza matumaini”.alisema mdede.
Lakini MDEDE aliwataka vijana kuwa mstari wa mbele
katika kuinua uchumi wa nchi.
MDEDE aliyasema katika
kongamano la vijana wa katoliki katika kata ya ulete Iringa vijijini ambapo
amewataka vijana kutambua umuhimu wao katika jamii ili kuleta madadiliko chanya
kwa taifa .
Aidha Dkt MUSA amesema kuwa wazee ni hazina kwa taifa kwa ushauri wa
mambo mbali mbali ya kiuongozi lakini
nguvu ya vijana inahitajika ili kulikwamua taifa kutoka hapa lilipo na kusonga
mbele.
0 comments:
Post a Comment