Home » » WANAKIJIJI ITUNDU KATA YA MLANGALI WATAKA FILIKUNJOMBE KUENDELEA UBUNGEWAMCHANGIA TSH 65,200 ZA FOMU

WANAKIJIJI ITUNDU KATA YA MLANGALI WATAKA FILIKUNJOMBE KUENDELEA UBUNGEWAMCHANGIA TSH 65,200 ZA FOMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mwanamke  mkazi   wa kijiji  cha Itundu kata ya  Mlangali  wilaya ya  Ludewa akimchangia  mbunge  wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe wa pili  kushoto pesa ya fomu ya  ubunge wa kwanza kushoto ni katibu wake Bw Stany Gowele
Wananchi  wakimchangia mbunge  Filikunjombe pesa za kuchukua fomu ya ubunge
Mbunge Filikunjombe  akichangiwa  pesa  ya  kuchukulia  fomu ya  ubunge muda ukifika
Mbunge  Filikunjombe akifurahia  kuchangia pesa  ya kuchukulia  fomu ya ubunge
Wananchi wa kada mbali mbali  wakimchangia mbunge Filikunjombe
Filikunjombe akikabidhi sare  kwa madereva  boda  boda Mlangali
Kwaya  ya  vijana  wakiimba  wimbo  wa  kulinda amani  wakati wa mkutano wa mbunge Filikunjombe
Mbunge  Filikunjombe  akizungumza na  wananchi  wa kijiji  cha Itundu kata ya Mlangali Ludewa
Filikunjombe akitoa  mfano  wa mshikamano  wa  kimaendeleo  unavyoweza  kuleta mabadiliko makubwa
Mbunge  wa Ludewa Deo  Filikunjombe  akikabidhi   vifaa vya  michezo kwa timu zote 8 za  vitongoji  vya kijiji cha Itundu  kata ya Mlangali


Na matukiodaimaBlog,Ludewa


WANACHAMA  wa asasi  za  fedha   vijijini kutoka   vikundi zaidi ya saba  vya Vicoba na  Sliki pamoja na  wananchi  wa kijiji  cha Itundu kata ya  Mlangali  wilaya  ya  Kilolo mkoani Njombe  wamemchangia  mbunge wa  jimbo la  Ludewa  Bw  Deo Filikunjombe kiasi cha Tsh 65,200 kwa  ajili ya  kuchangia fedha  za  kuchukua  fomu ya  kuwania ubunge kwa muhula wa  pili katika  jimbo  hilo la Ludewa.


Pamoja na  kuchangia   pesa  hiyo  pia   wakazi wa kata   hiyo  kupitia   wazee  wa kijiji  cha  Itundu  walikitaka  chama  cha  Mapinduzi (CCM) kutoruhusu wana CCM wengine  kuchukua fomu ya ubunge katika   jimbo la Ludewa ili wao  kuweza  kuendelea na  mbunge  wao  wa  sasa  kutokana na  utendaji kazi  wake kiasi cha  kuwakomboa  wananchi  wa Ludewa .


Wananchi  hao  waliyasema  hayo  jana   kwa nyakati  tofauti wakati  wa   hafla  ya uziduzi wa vikundi hivyo  na mkutano  wa hadhara  uliofanyika katika  viwanja wa Stendi katika  kijiji  hicho cha Itundu .


Mzee  Augustino Msemakweli  na mzee Herbert Kayombo   walisema  kuwa  ni  mbunge  wa kwanza kwa  jimbo hilo la  Ludewa  kati ya  wabunge  zaidi ya 6  waliopata  kuongoza kufanikisha  utekelezaji  wa ahadi zake kwa  wakati na  kuwa wao kama  wazee wa kijiji  hicho na  ni miongoni mwa  wazee wa jimbo la Ludewa ambao ni makada wa CCM kilio chao  kwa  sasa ni kuona mbunge  huyo anaendelea  kuongoza jimbo  hilo zaidi  pamoja na kuwasaidia kuwapigania  wazee  ili kuweza  kuliptwa mafao  ya uzeeni kutoka  serikalini.


Mzee  Msemakweli  alisema  kuwa  amepata  kusoma moja kati ya gazeti la wiki  kutoka Zanzibar  na  kuonyesha ni kiasi gani serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar  ilivyoweka mkakati  wa kuwasaidia  wazee  kwa  kupanga  kumlipa mafao mzee  kila mwezi  kiasi cha kuanzia Tsh 20,000 hivyo  kuomba mbunge  wao kuendelea  kuungana  na  wabunge wengine  ili nao  waweze kulipwa mafao ya uzeeni.


Wakati   mzee Kayombo  akieleza kufurahishwa na utendaji wa Filikunjombe na  kusikitishwa na mbinu  chafu za upinzani katika kata   hiyo  inayoongozwa na diwani  wa chadema na mwenyekiti  wa Chadema kuwazuia wananchi kulima katika mabonde ( Vinyungu)na  kuwa  wanafanya  hivyo  kwa  lengo la  kukwamisha jitihada za  mbunge wao.

Kwani  alisema  katika  kijiji  hicho wananchi miaka  yote  walikuwa  wakilima kwenye  vinyungu  kutokana na  eneo hilo  kutokuwa na chanzo  cha maji na  hata  umeme  wanaotegemea  kupata  hauzalishwi katika  kijiji  hicho  .

Alisema  kuwa serikali ya  kijiji  inawataka  wananchi  kutolima umbali  wa mita 60 ya  mto  wakati umbali  huo ni mkubwa  ukilinganisha na ukubwa wa  eneo   hilo.


Kuhusu mtazamo  wa  wananchi  wa  Ludewa juu ya utendaji kazi wa mbunge  huyo alisema  wao kama  wazee wamefurahishwa na kazi  zinazofanywa na mbunge  huyo na  kuwa wao kama  wapiga kura wanahitaji mtu na  sio  chama na kama chama kitaona Filikunjombe hawafai  wao kama  wananchi hawatakuwa tayari kuunga mkono maamuzi  yoyote  nje ya matakwa  yao.


Hata   hivyo  alisema  kuwa changamoto  kubwa ya  kijiji  chao kwa sasa ni maji na umeme na kumshukuru mbunge kwa  kuwasaidia  gari la  wagonjwa katika  kijiji na kata yao  ya Mlangali .


Kwa  upande wake Emmanuel Mpogole akizungumza kwa niaba ya wanachama  wa vikundi  vya kifedha  vijijini alisema  kuwa kumekuwepo na hamasa  kubwa ya uanzishwaji  wa  vikundi  hivyo toka  alipoingia mbunge  huyo madarakani na kuwa hali ya  uchumi wao  imezidi  kuboresheka  zaidi.


Akizungumza na  wananchi hao  mbali  ya kuwashukuru kwa mchango wao wa  fedha za  kuchukulia fomu Bw  Filikunjombe alisema kuwa  imani ambayo  wananchi  wanaionyesha kwake ni  kubwa na kuwa mbali ya  kutumia kiasi cha Tsh  milioni 75 kwa wilaya  nzima kila mwaka  kusomesha  watoto zaidi ya 20  kila kata  bado kata   hiyo ya Mlangali  ndio kata  pekee ambayo  mmoja kati ya  wanafunzi aliowasomesha  alifika kushukuru na   hivyo kwa mwaka   mwakani kata  hiyo atasomesha  watoto 30 badala ya 25 kama kata  nyingine.


Pia  alisema suala la maji bado  wa kulaumiwa ni  viongozi wao wa  kijiji ambao hata katika taarifa ya kijiji kwa mbunge hawaonyeshi kama  wana tatizo la maji kama  viongozi wa vijijini  vingine ambao taarifa  zao  hueleza  wazi changamoto mbali mbali .

Bw  Filikunjombe  alisema mbali ya viongozi wao kutoeleza tatizo hilo la maji ila kwa upande wake analichukua  ili  kuanza kushughulikia kumaliza   kero ya maji katika  kijiji  hicho .


Mbunge  huyo katika  kuunga mkono  vikundi vya   kifedha  vijijini aliahidi  kusaidia  kutoa mafunzo  ya ujasliamali kwa  wanachama  wote  wa vikundi  zaidi ya 7 vya  kifedha  vijijini pamoja na  kila  kikundi kukichangia kiasi cha Tsh 500,000 huku  kikundi  cha boda boda akikichangia kiasi cha Tsh milioni 2.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa