Home » » Prof Mwandosya; Mwaka 2005 nilikuwa wa tatu mwaka huu ikulu zamu yangu, ataka wagombea wenzake wasiogope kuelezwa maovu

Prof Mwandosya; Mwaka 2005 nilikuwa wa tatu mwaka huu ikulu zamu yangu, ataka wagombea wenzake wasiogope kuelezwa maovu

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri asiye na Wizara maalum Prof Mark Mwandosya akiwapungua mkono baadhi ya wahudumu wa uwanja wa Ndege wa Nduli Iringa wakati akiondoka mkoani Iringa kuelekea mkoani Tabora kutafuta  wadhamini kwa ndege hiyo ya kukodi.
Waziri Prof Mwandosya  akitafakari jambo.
Dereva  wa gari la Prof Mwandosya  Iringa akipata picha ya kumbukumbu na kuagana na rubani wa ndege aliyokodi Waziri huyo.
Wadhamini wa Prof Mwandosya  wakiagana na waziri huyo.
Waziri Prof. Mwandosya  na mkewe akishuka katika gari la kukodi jana ofisi  za CCM wilaya ya Iringa  vijijini.


Waziri Prof Mwandosya akizungumza na wanahabari mkoa wa Iringa.
DSC_0821
Mke wa waziri Prof Mwandosya, Katibu msaidizi wa CCM Iringa vijijini Bw. Jackson na Waziri Prof Mark Mwandosya wakisikiliza maswali ya wadhamini.
Baadhi ya  wadhamini  wa waziri Prof Mwandosya.
Katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Bw Hakim Jackson (kushoto) akimkabidhi Prof Mark Mwandosya fomu yenye majina ya wadhamini wake mkoani Iringa.
Mwenyekiti  wa UWT wilaya ya  Iringa  vijijini Shakra Kiwanga akimpongeza Prof Mwandosya.
Prof Mwandosya na mkewe wakiingia katika ndege tayari kwa  safari ya kwenda mkoa wa Tabora na Kigoma.
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI asiye kuwa na  wizara maalum Prof Mark Mwandosya ambae ni  mmoja kati ya  wana chama wa chama cha mapinduzi zaidi ya 35 walijitokeza  kuchukua  fomu za  kuomba kuteuliwa  kuwa  wagombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM amesema  kuwa baada ya mwaka 2005 kushika nafasi ya tatu katika kinyang’anyiro cha Urais ni matumaini  yake mwaka huu atafanya vizuri zaidi kwa  kushika nafasi ya  kwanza kati ya  wote  waliojitokeza sasa.
“Wewe una  mtoto anasoma  darasa  la tatu  mfano na darasa  kati  ya  watoto 90 yeye  amekuwa  wa tatu ukiwa kama mzazi lazima utampongeza na kumweleza  kuwa uongeza jitihada  na mtihani  ujao baada ya  kuongeza jitihada kuwa mwanangu  nataka mtihani ujao  uwe  wa kwanza  sawa anakujibu   sawa ……sasa  mimi mwaka 2005  nilikuwa  wa tatu sasa unataka  kuniambia  nini tena”alihoji Prof Mwandosya  huku wote  wote pamoja na wanahabari  wakiangua kicheko .
Akizungumza na  wanahabari  leo katika  ofisi ya  CCM wilaya ya  Iringa  vijijini mara  baada ya  kudhaminiwa na  wanachama 28  wa CCM ,Prof Mwandosya alisema  kuwa safari  yake ni safari ya uhakika na  hivyo iwapo  chama chake  kitamteua kuwa  mgombea watanzania wategemee kuwa na nchi yenye uchumi  bora .
Prof Mwandosya ambae  aliulizwa na  wanahabari hao  kuwa anajambo gani jipya la kulifanya ambalo Rais anayemaliza  muda  wake Dr Jakaya Kikwete hakufanya alisema  kuwa  si  kweli kama serikali ya Dr Kikwete haikufanya  lolote japo alisema kiwa awamu ina changamoto  zake na kila awamu imefanya mambo makubwa.
“Kusema unalinganisha  na  serikali  iliyopo ni kama  vile  unataka  kusema serikali  zilizotangulia hazikufanya  lolote ama hazikufikia  malengo yaliyotarajiwa  ukweli  ni  vipindi  katika  uongozi  wa nchi  ambavyo vinatofautiana  mfano miaka  iliyopita  mimi nikiwa  waziri  wa mawasiliano na  uchukuzi simu  hizi  za  mikononi ambazo matumizi yake ni makubwa hazikuwepo ila  sasa  kuna  simu ambayo ni kamera ,Voice recoda na pia  ni kopyuta  hiyo  hiyo  sasa huwezi  linganisha  miaka hiyo na  sasa na huwezi  sema serikali iliyopita haikufanya ukweli kila  serikali imefanya kulingana na wakati wake.”
Alisema kuwa atafanya zaidi ya serikali  iliyopita ama  chini ya  serikali iliyopita bado  si  jibu la kumsaidia mtanzania kwani  alisema  katika ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005 -2010 ujenzi  wa  chuo kikuu  cha Dodoma haukuwepo na wala haikuwa ni ahadi ya Rais Dr  Kikwete  ila kutokana na kuna kuna haja ya  kuanzisha  chuo  hicho serikali  iliweza kuadhimia na  kufanikiwa  kuanzisha  chuo  hicho ambacho ndicho  chuo bora nchini na Afrika Mashariki .
Hata hivyo  alisema  kuwa kwa  kuwa kipaumbele  chake  kikubwa ni  kujenga uchumi bora  pia ana amini kupitia uchumi bora  hakuna jambo litakaloshindikana kwani katika uchumi bora itakuwa ni  vigumu kuzungumzia  uchumi  bora kama miundo  mbinu haitaboreshwa  wala bila kuwepo kwa  kilimo na masoko  ama  kuwa na masoko  bila  viwanda au kuzungumzia kukuza  uchumi bila  kuwa  na elimu bora.
Prof Mwandosya alisema  kuwa mbali ya  kuwa ni  waziri ila bado anaishi na jamii na pia anatambua mazuri  mengi  yaliyofanywa na Rais Dr  Kikwete na  changamoto  zake   hivyo akiingia  Ikulu lazima yale mazuri  yote yaliyofanywa na serikali  iliyopita atayaendeleza  zaidi  ya hapo yalipoachiwa na zile  changamoto  kuweza  kuzitafutia majibu  sahihi kwa faida ya  jamii ya  kitanzania.
Pia alisema mambo  mengi anayatambua vema kwa  kuwa  yupo  jikoni na mengine anayatambua vizuri  kutoka kwa jamii ambayo imemlalamikia  hivyo jukumu la kuyatekeleza lipo  mikononi mwake na kuwataka  wananchi hasa wana CCM kuendelea kujenga  imani zaidi kwake .
“Lazima  kuwa na vipaumbele ambavyo  ni majibu ya mwananchi katika kukuza  uchumi kwani  huwezi chukua elimu ukaacha  miundo  mbinu kwani miundo  mbinu ndio  itakuza uchumi na  huwezi  zungumzia afya  bila kuboresha elimu ….ukifanya haya makubwa manne hapo ndipo unageukia upande  wa pili…..niseme  tu kuwa uchumi unapokuwa lazima unazungumzia takwimu na  kuona kipato  cha Taifa  kinaongezeka”
Waziri Prof Mwandosya  alisema kuwa katika utawala  wake kama Rais ni  kuona anakuza  uchumi  zaidi kupitia  kilimo huku akiamini  kuwa  asilimia zaidi ya 80 ya watanzania  wanategemea  zaidi  kilimo katika  kuendesha maisha  yao na  kilimo pia kinaweza  kukuza  uchumi  haraka  zaidi .
Katika hatua nyingine Prof Mwandosya amewataka  wagombea wenzake kuheshimu taratibu  za CCM katika mchakato  wa  kutafuta  wadhamini badala ya kugeuza mbio hizo kama   sehemu ya kuonyesha umarufu usio na tija na kuwa utaratibu wa CCM ni  kupata wadhamini 450 pekee pasipo mbwembwe  za aina  yoyote pia vigezo  vya mgombea  wa  urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania vipo wazi  kuanzia kiwango  chake cha elimu na awe na miaka kuanzia 40 kuwataka wote watia nia kujitathimini badala ya  kuingiza mchezo katika  suala  hilo nyeti.
Prof Mwandosya aliwataka  wagombea wenzake  ndani ya CCM wasilalamike kwa kukumbushwa ukweli na madudu waliyoyafanya wakati  wakiwa  serikalini kwani ni  vigumu watanzania  kusahau maovu ya mgombea yeyote na  kuwa anachojivunia yeye katika uongozi  wake toka kipindi  cha hayati baba wa Taifa hadi sasa hajapata  kuwa na sifa mbaya kama baadhi ya wagombea  wengine ambao wamechukua fomu ya  kuomba kuaminiwa na CCM mbali ya kuwa na sifa mbaya kwa Taifa
Pia alieleza  kusikitishwa na matumizi makubwa ya pesa katika mchakato huu na kuwa anashangazwa kuona wana CCM wakiendelea kuchezea pesa kwa kuandaa mbwembwe nyingi mikoani kwa ajili ya mapokezi yao wakati kila mgombea alipewa taratibu na chama juu ya nini afanye wakati  wa kuzunguka kutafuta  wadhamini na  kuwa pesa  zinazotumia zingeweza kusaidia miradi ya  kijamii kuliko kuzimwaga kama njugu kwani ni hatari kwa uhai  wa chama .

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa