katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akiwahutubia wananchi wa tarafa ya pawaga.
katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akijibu maswali ya wananchi wa tarafa ya pawaga.
katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akiwapa vifaa vya michezo wananchi wa tarafa ya pawaga
na fredy mgunda,iringa
katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa iringa hassani mtenga amewataka wananchi wa tarafa ya pawaga katika
jimbo la isimani kuendelea kumwamini mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa anawatendea
haki kwa kuwaletea maendeleo.
akizungumza katika mkutano huu katibu wa chama hicho MTENGA amewataka wananchi kuendelea kukiamini chama
hicho kutokana na kutekeza ahadi zao ambazo wanakuwa wanaziahidi kwa wananchi.
Kwa upande wao wananchi kijiji cha boliboli kilichopo tarafa
ya pawaga wilaya ya iringa vijijini
wanakabiriwa na matatizo ya kiafya pamoja na migogoro ya aridhi baina ya
wafugaji na wakulima hayo yamebaini katika mkutano ulifanyika katika kijiji
hicho.
wakizungunza wakati wa mkutano huo wananchi hao wamesema
kuwa kijiji hicho hakina mganga wa kutoa
huduma katika zahanati yao na kuongeza kuwa tatizo la migogolo ya aridhi
limekuwa kubwa.
Akijibu maswali ya wananchi hao katibu wa ccm mkoa wa iringa
hassani mtenga amewata viongozi wa chama hicho kufanya mikutano ya
mara kwa mara na kupokea kero za wananchi na kuzitatua mapema ili kuendelea
kukijengea imani chama chao.
Viongozi wengi wamekuwa hawawajali wananchi wao ambao
wamewaweka matarakani na ndio imekuwa sababu ya matatizo mengi na migogolo
mikubwa katika vijijini.
Lakini MTENGA amesema swala mfureji,tatizo la mganga,walimu
kuwa walevi na mgogoro wa mbomipa anayachukua na kwenda kuyafanyia kazi na
kuwaahidi kuwa matatizo yote waliomweleza yatatulika.
“Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuipigia kura katiba
inayopendekezwa ili waweze kupata katiba ya wananchi na kuwaambia wananchi wa
eneo hilo kuitumia fursa ya kuijiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia
kura ambalo iringa litaanza tarehe 29 mwezi huu” alisema HASSAN MTENGA.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment