Home » » MBUNGE WA JIMBO LA KALENGA AKABIDHI MADAWATI 30 NA TSH MILIONI 36KUCHANGIA UJENZI WA MAABARA‏

MBUNGE WA JIMBO LA KALENGA AKABIDHI MADAWATI 30 NA TSH MILIONI 36KUCHANGIA UJENZI WA MAABARA‏



Mbunge  Mgimwa  akimkabidhi  madawati diwani wa kata ya Mgama Bw  Lupala
Mbunge  Mgimwa  akikabidhi  madawati  30  kwa  viongozi wa  serikali ya  kijiji  cha Lwato  kata ya Mgama
Mbunge  Mgimwa  akisalimiana  na  wananchi  wa kata ya  Mgama
Mzee  mkazi wa Mgama  akimweleza  jambo  mbunge  Mgimwa
Mbunge  wa  jimbo la  Kalenga  Godfrey Mgimwa  kulia akisaidiana na diwani wa kata ya Mgama Bw  Denis Lupala  kushusha madawati katika  lori  kwa  ajili ya shule ya msingi Lwato
Mbunge wa  jimbo la kalenga  akiwa katika  usafiri  wa Baiskeli  kuelekea  katika kukagua  miradi ya maendeleo kata ya Mgama
Mbunge wa Kalenga  wa  tatu  kulia akiwa  na  wadau wa maendeleo  kata ya Mgama
Mbunge wa kalenga  Bw  Mgimwa  akimkabidhi msaada wa  pesa  diwani wa kata ya Mgama Bw Denis Lupala kwa ajili ya  kusaidia  kununua mifuko ya  20 ya  saruji  ili  kukamilisha  ujenzi  wa  choo katika zahanati ya Itwaga  ambayo  imeshindwa  kuanza kazi  kutokana na ukosefu wa  choo
Wananchi  wa Mgama  wakiwa katika mkutano  wa hadhara wa mbunge  Mgimwa
Wananchi wa Mgama  wakizuia  msafara wa mbunge  Mgimwa  kwa furaha ya  kupelekeza  umeme 
Na  Matukiodaima Blog
Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa amekabidhi madawati 30 kwa shule ya msingi  Lwato kata ya Mgama huku akiwataka wananchi kutodanganyika na wanaojipitisha Kwani bado anautaka ubunge tena ila kuzidi kuwatumikia.

Akizungumza na  wakazi  wa  vijiji  vya kata ya  Mgama  kwa  nyakati   tofauti  jana  baada ya  kukabidhi  msaada  wa  madawati kwa   shule  ya  mpya ya  msingi ya  Lwato kama  sehemu ya  utekelezaji  wa ahadi  yake  ,mbunge  Mgimwa  alisema bado  anautamani  ubunge  hadi  hapo  dhamira  yake ya  kimaendeleo  itakapo  timia.

Hivyo  alisema lengo  lake  ni  kuhakikisha  anatekeleza  ahadi  zote  zilizoachwa na  mbunge  aliyetangulia  mbele za haki  Dr  Wiliam  Mgimwa   kabla ya muda  wa  kuvunja  bunge   kufika  na  kuwa kwa  sehemu kubwa tayari  ahadi  hizo  amezitekeleza .

Alisema  kuwa  amepata  kutekeleza  ahadi  mbali mbali  zilizoachwa na  mbunge  aliyetangulia  katika  jimbo  hilo la  Kalenga  kwa kipindi   kifupi  zaidi  kutokana na kuwa na moyo  wa  kuwatumikia   wananchi  wa  jimbo  hilo la Kalenga kwa  kipindi  kijacho  baada ya  uchaguzi  mkuu  wa  Octoba  mwaka  huu.

" Wapo  baadhi ya  watu  wanajipitisha  pitisha na kudanganya  wananchi kwa  kuwahonga  pesa   kwa  madai  kuwa mimi sitagombea  ubunge  tena  wa kalenga ......leo  nawahakikishieni kuwa mimi  nitagombea  tena  ubunge  mwaka  huu ili   niweze  kuwatumikia    zaidi  baada ya  huu ubunge  wangu  wa  mwaka  mmoja  kumalizika .......umri    wangu bado  unaruhusu  kuendelea kuwatumikia hadi  vipindi  vinne  ama   zaidi  mimi  bado  kijana na pia nimesoma  najitambua  zaidi .....wanaowatenga kwa  kuwahonga  wachache  pesa wacha  waendelee ila  mimi nitahakikisha naendelea kuwaletea maendeleo wananchi  wote  bila  kujali itikadi  za  vyama vyetu"


Awataka kutoacha kupokea pesa za wagombea wanaojipitisha ila msimamo wao ni kumchagua mbunge wa maendeleo badala ya mgombea mwekezaji ambae anagawa pesa na riba yake kuichukua Baada ya kuwa mbunge 

Mbali ya kuchangia madawati hayo pia mbunge huyo amechangia kiasi cha Tsh Milioni 36 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara katika shule mbali mbali za sekondari jimbo la Kalenga huku  jumla  ya  zaidi ya  Tsh milioni 500 zikitumika  katika  miradi  mbali mbali ya  kimaendeleo katika   jimbo  hilo  toka  alipoingia  madarakani  mwaka  jana.

Aliyataja  baadhi ya maeneo  ambayo  amekuwa  akisaidia  kuwa ni  pamoja na uendelezaji  wa ahadi  za mbunge  aliyetangulia  kwa  kuwawezesha  wananchi  kufungua  VICOBA  zaidi  na  kuwa toka  amekuwa mbunge  jumla ya    vikundi  vya  VICOBA 30  amevianzisha  na  kuviunga  mkono kwa  kuchangia  fedha .

Kwa  upande  wake  diwani wa kata ya  Mgama  Bw  Denis  Lupala  akishukuru  kazi  za mbunge   huyo alisema  kuwa  jimbo la Kalenga halina  sababu ya  kuendelea  kubadili  wabunge  kama  nguo na  kuwa  kwa  muda  mfupi ambao Bw  Mgimwa amepata  kuwa mbunge  wa  jimbo  hilo kasi ya maendeleo  imekuwa ni  kubwa  zaidi.

Lupala ambae  pia ni katibu  wa itikadi na uenezi  wa  wilaya ya  Iringa  vijijini  alisema  atahakikisha anashawishi  wananchi  wa  Kalenga  ili  muda  ukifika   kwa  kauli  mmoja  kumpitisha  tena  Mgimwa  kuwa  mgombea pekee  wa  jimbo   hilo kutokana na kipimo  cha  utendaji kazi  alichokionyesha  kwa  muda  mfupi  wa majaribio  kwake .

Alisema  moja kati ya ahadi  yake  kubwa katika  kata  yake ya  Mgama  ilikuwa ni umeme na tayari  hadi  sasa ahadi  hiyo  imetekelezeka kwa  nguzo  za  umeme na  nyaya  kusambazwa  katika eneo  hilo la Mgama pia  madawati  katika  shule ya msingi Lwato  ametekeleza  na  shughuli  nyingine  nyingi .

Akizungumza  kwa  niaba  ya  wananchi wa kata   hiyo  ya  Mgama  Bw  Obadia  Sanga  alisema  kwa wananchi  wa Kalenga  kwa  sasa  wamekua na hawapo tayari  kuendelea  kulifanya  jimbo  hilo  kuwa la watu  kujifunzia  ubunge ama kuwafanya  wananchi  ni mtaji wao  wa  kiuchumi  hivyo kwa mwaka  huu   hawataki michepuko wataendelea  kubaki  njia kuu  kwa  kuwa na mbunge   huyo tena  ili  kuendeleza jimbo la Kalenga.

Alisema  wapo  baadhi ya  watu  wanapita  na  kutengeneza  matabaka  katika jimbo  hilo la Kalenga  kwa  kuwatumia wachache kuwapa  pesa  ili kuwashawishi  wananchi na mbaya  zaidi  wamekuwa wakiponda kazi  kubwa  inayofanywa na mbunge  wa CCM huku  na  wao ni  wana CCM jambo ambalo ni hatari  zaidi kwa uhai  wa CCM iwapo mwana CCM badala ya  kupongeza  utekelezaji wa ilani ya  CCM anaishia  kuponda wakati wao wapinzani wamekuwa  wakipongeza kazi   hizo  zinazofanywa na Mgimwa .
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa