Home » » ‘WANAWAKE CCM MSIWACHAGUE VIONGOZI WATOA RUSHWA’

‘WANAWAKE CCM MSIWACHAGUE VIONGOZI WATOA RUSHWA’

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga amewataka wafuasi wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho mkoani hapa kutowachagua viongozi wapenda rushwa kwa kuwa ni chanzo cha kukosa imani kwa serikali yao.
Mtenga alisema hayo juzi alipozungumza na wanachama wa umoja huo katika kikao cha kawaida kilichofanyika mjini hapa jana na kusema wananchi wanahitaji maendeleo hivyo kubainisha kwamba viongozi wanaoingia kwa misingi ya rushwa hawezi kuwaletea maendeleo ya wananchi.
Alisema wanawake ni nguzo kubwa ndani ya CCM hivyo wakimchagua kiongozi mtoa rushwa watajikosesha maendeleo huku akisisitiza kwamba viongozi wa aina hiyo hawatakiwi katika jamii.
“Wanawake mna nguvu ndani ya chama lakini nyie ndio mtakaofanya kosa kuwachagua wenye mikono mirefu na kuwaacha wenye nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi… mfano akitokea nyoka amewekwa fedha mwili mzima mpo tayari kwenda kuchukua fedha hizo?
“…Ifike mahala sisi watu wa chini kujisahihisha kwa kuwa tunaweza kuwapa wananchi viongozi wenye nia dhabiti ya kuleta maendeleo,” alisema Mtenga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja huo mkoani hapa, Zainabu Mwamwindi alisema ushirikiano, upendo  na mshikamano ndani ya chama ni msingi wa mapambano katika kuelekea chag
  Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa