Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MBUNGE
wa Kilolo, Profesa Peter Msola, amewataka wananchi wa jimbo hilo
kuwekeza katika elimu kwa kupeleka watoto shule ili kuondokana na janga
la kukosa elimu.
Profesa Msola aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kilolo
katika Kijiji cha Mwatasi, wakati wa ziara ya siku moja na kusisitiza
umuhimu wa wazazi kuwaelimisha na kuwapatia watoto wao elimu.
Msola alisema kuna wazazi ambao wanashindwa kuwekeza katika elimu na
kuwafanya watoto kukimbilia mijini ambako hukutana na maisha magumu ya
kuombaomba kutokana na kutokuwa na elimu.
Alisema kuwa maendeleo miongoni mwa jamii yanachangiwa kwa kiasi
kikubwa na kiwango cha uwekezaji katika elimu, hivyo ni vyema jamii
iwekeze katika sekta hiyo ili kujikwamua na umaskini uliopo na kupambana
katika soko la ajira.
“Tukumbuke kwamba kuwekeza katika elimu ni mkakati wa muda mrefu
unaohitaji dhamira, subira na kwamba matokeo yake huonekana baada ya
muda mrefu wa uwekezaji na faida kwa wazazi mara baada ya mtoto kusoma
na kuweza kumsaidia pindi azeekapo,” alisema Prof. Msola
Prof. Msola alisema Kilolo ina rasilimali nyingi zinazohitaji
viongozi wabunifu watakaohakikisha zinatumika kwa faida ya wananchi.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment