Bw Jackson Kiswaga akijaribu kufungua koki ya maji kama ishara ya kuzindua rasmi huduma ya maji katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospital ya wilaya ya Iringa |
Hapa Bw Kiswaga akipongeza kwa jitihada zake za klimaendeleo jimbo la kalenga |
Hiki ndicho chumba cha kuhifadhia maiti ambacho Kiswaga amejitolea kuingiza maji |
Na Francis Godwin Blog
MKAZI
wa Nyamihuu jimbo la kalenga wilaya ya Iringa vijijini Bw Jackson
Kiswaga ametekeleza ahadi yake ya kusaidia kuingiza maji ya bomba
katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospital teule ya wilaya ya
Iringa (Ipamba) baada ya chumba hicho kukosa bomba toka Hospital hiyo
ilipoanzishwa .
Kiswaga
ambae kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam ametekeleza ahadi hiyo
ukiwa ni muda mwezi mmoja toka alipotembelea Hospital hiyo kwa lengo
la kusaidia msaada wa vitanda vya kujifungulia kwa wanawake na
kukutana na kero hiyo ya chumba hicho cha kuhifadhi maiti kukosa
huduma ya maji ya kuoshea maiti .
Akizungumza
baaada ya kutembelea kuzindua rasmi maji hayo jana Kiswaga alisema
kuwa amelazimika kutekeleza ahadi hiyo ya maji kutokana na maombi ya
viongozi wa Hospital hiyo juu ya huduma hiyo ya maji.
Kwani
alisema hakujisikia vizuri kuona chumba hicho hakina huduma ya maji
hivyo kujitolea kwake kuweka maji ya bomba kutoaondoa adha kubwa ambayo
ndugu walikuwa wakiipata ya kuchota maji katika ndoo na kutumia
kuoshea maiti katika chumba hicho.
katika
hatua nyingine Kiswaga ameahidi kuboresha zaidi eneo hilo la
chumba cha kuhifadhia maiti ikiwa ni pamoja na kujenga banda maalum
la ngudu kusubiri wakati maiti ikiandaliwa .
Alisema
kuwa akiwa akiwa kama mwana kalenga ataendelea kuwa karibu na
Hospital hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa wana Kalenga na ndugu
zake waliopo Kalenga hivyo iwapo ataiboresha zaidi itakuwa ni mwanzo
mzuri wa wananchi kupata huduma bora zaidi.
Kwa
upande wake mmoja kati ya wana kalenga waliolazwa katika Hospital
hiyo Bw Simon Sanga alimpongeza Kiswaga kwa jitihada zake na kuwa
wao toka miaka ya 1980 ambapo Hospital hiyo ipo hawajapata kuona
kiongozi awaye yeyote anayezungumzia kutatua kero ya maji katika
chumba hicho cha kuhifadhi maiti na tayari viongozi mbali mbali ambao
walitangulia mbele ya haki wamepata kuhifadhiwa miili yao katika
chumba hicho.
Mbali
ya kumpongeza Kiswaga pia alisema kati ya wabunge wote waliopata
kuongoza jimbo hilo la kalenga hakuna mbunge hata moja ambae
ameonyesha kuliona tatizo la maji ambalo Kiswaga amelitatua na
kumtaka mbunge wa jimbo hilo Dr Wiliam Mgimwa badala ya kuendelea
kuwabeza wanaojitolea kuchangia maendeleo ya jimbo la Kalenga pia
kujaribu kuisaidia Hospital hiyo ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wana
kalenga wanaoishi nje ya jimbo hilo ambao wameendelea kujitolea
kusaidia maendeleo ya wana Kalenga
0 comments:
Post a Comment