Mtu mmoja
anayetuhumiwa kuwa jambazi ameuawa na mwingine akikamatwa wakati wakivamia duka
la Santino Mdesa katika kijiji cha Mkonge kilichopo katika Wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa, huku wahamiaji haramu watano kutoka nchi ya Ethiopia wakikamatwa
kwa kosa la kuingia nchini pasipo kufuata taratibu.
Akizungumzia tukio hilo ujambazi, kamanda wa
jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Athmani Mungi amesema majambazi hao
walifyatua risasi hewani ambapo wananchi walipobaini uwepo wa tukio hilo la
Uharifu walizingira eneo hilo ambapo majambazi walitambua mbinu hizo na kukimbia.
Aidha kamanda Mungi amesema wananchi kwa
kushirikiana na askari polisi waliwakimbiza majambazi hao na baada ya kuzidiwa
nguvu, majambazi walitupa bunduki aina ya SMG iliyokuwa na Lisasi 21, na kisha
kutelekeza usafiri wao wa Pikipiki, huku askari wakifanikiwa kumpiga kwa risasi
mguuni jambazi mmoja aliyekufa wakati akipelekwa kupata matibabu.
Mungi amesema pia Polisi wamefanikiwa kumkamata
mwananchi wa kijiji cha Kitayawa katika Wilaya ya Iringa ambaye amekuwa
akitengeneza Bunduki za kienyeji.
Katika tukio lingine kamanda Mungi amesema,
wamewakamata wahamiaji haramu watano kutoka nchi ya Ethiopia ambao walikuwa
wamejificha katika poli la mashamba ya kijiji cha Mazombe, katika Wilaya ya
Kilolo mkoani Iringa, na kuwa wahamiaji hao walikuwa wanaelekea nchini Afrika
Kusini.
Akithibitisha kukamatwa kwa wahamiaji hao
haramu, ofisa uhamiaji mkoa wa Iringa Ali Nassor amesema wahamiaji hao haramu
wakiethiopi wapo chini ya ulinzi kwa hatua zaidi.
0 comments:
Post a Comment