![]() |
Jinsi Daudi Mwangosi alivyouawa |
=============================================
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mufindi imetupilia mbali mashtaka ya
yaliyokuwa yakiwakabili Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Hamad Yusuph na wenzake 42.
Kiongozi huyo pamoja na wenzake walikuwa
wakikabiliwa na makosa matatu likiwemo la kufanya mkutano bila kibali
pamoja na kuharibu mali ambazo ni kofia za pikipiki (helmenti) 2 za
polisi katika tukio lililosababisha kuuawa aliyekuwa mwandishi wa habari
wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daudi Mangosi katika kijiji
cha Nyololo wailayani Mufindi.
Kutokana na tuhuma hizo Chadema iliweka pingamizi za kutaka kesi hiyo ifute kwa kuwa ilifunguliwa kinyume cha sheria.
Wakili
wa Chadema Lugaziya akisaidiana na mwanasheria wa Chadema Luka Sinkala
Mwenda waliweka pingamizi dhidi ya kesi hiyo .
Pingamizi lingine ni kwamba aliyetoa amri ya
kutawanya mkutano hakuwa na cheo chochote, wakati Chadema ikizuiliwa
Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Bububu Zanzibar walikuwa na
mkutano wa kampeni za uchaguzi, polisi walisema wanazuia mkutano kwa
kuwa sensa inaendelea wakati huo sheria ya uchaguzi haizuii shughuli
zingine kufanyika na kwamba walitaka polisi waeleze sheria ya sensa
inayozuia shughuli zingine kufanyika inatoka wapi.
Watuhumiwa hao walikamatwa maeneo ya Igawa mpakani
mwa Mkoa wa Iringa na Mbeya baada ya kutoka katika eneo waliloamriwa
kutawanyika.
Hakimu
wa Wilaya ya Mufindi D. Nyakunga alisema pingamizi zilizowasilishwa na
Chadema hazikujibiwa hata moja na upande wa utetezi.
"Hakuna pingamizi yoyote iliyojibiwa na upande wa
utetezi. hivyo na kuwa hayo ni matumizi mabaya ya kifungu namba 91 kinataka upande wa
utetezi kujibu pingamizi.
"Pia ni matumizi mabaya ya muda na fedha za serikali za walipa kodi. Kwa sababu zote hizo, kesi hii inafutwa" alisema Nyakunga.
Naibu
Katibu Mkuuwa wa Chadema Zanzibar Hamad Yusuph na wenzake walifunguliwa
kesi hiyo baada ya kukamatwa wakati wa ufunguzi wa matawi Septemba 2,
2012 ambapo mwanahabri wa Chanel Tena na mwenyekiti wa Klabu ya
waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi aliuawa na
polisi kwa kupigwa bomu.
NA FRANCIS GODWIN
0 comments:
Post a Comment