Hali ilivyo nje ya kiwanda hicho |
Wakati Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imefanikiwa kuwa mshindi wa
pili katika tuzo ya usafi wa Mazingira kitaifa mwaka 2013 ikiongozwa
na Halmashauri ya Moshi iliyoshika nafasi ya kwanza hali imeanza kuwa
tofauti katika kiwanda cha Dabaga Vegetable kutokana na uchafu
uliokithiri kiwandani hapo .
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa www.matukiodaima.com na www.francisgodwin.blogspot.com umebaini kuwepo kwa hali mbaya ya uchafu katika kiwanda hicho na iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa upo uwezekano wa magonjwa ya mlipuko kujitokeza katika eneo hilo.
Tayari wananchi wameitupia lawama ofisi ya afya manispaa ya Iringa kuwa imeshindwa kazi kutokana na kushindwa kufuatilia uchafuzi huo wa mazingira eneo hilo.

Picha na Francis Godwin
0 comments:
Post a Comment