Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma akizungumza na wanahabari jioni la leo ofisini kwake
Wanahabari Iringa wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa akisikiliza maswali ya wanahabari waliofika kumsikiliza
Baadhi ya wanahabari mkoa wa Iringa wakitoka kumsikiliza mkuu wa mkoa leo
Mmiliki wa mtandao huu mzee wa
matukio daima akiandaa kipindi kwa ajili ya kituo cha runginga cha
Manispaa ya Iringa (IMTV) baada ya kutoka kwa mkuu wa mkoa mpiga
picha ni Vicent Msigwa jembe
SERIKALI mkoa wa Iringa imepinga vikali
taarifa za upotoshaji zilizotolewa na kituo kimoja cha TV hapa
nchini kuhusu kuwepo kwa maandamano ya wakulima wa mpunga Pawaga
ambao wanapinga ushuru wa mazao na kuwa habari hiyo haikuwa na ukweli
kwani waliofanya maandamano hayo ni wafanyabiashara wa mpunga ambao
walivaa kofia za wakulima ili kuendelea kuwanyosha wakulima.
Akizungumza na wanahabari leo ofisini
kwake mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma alisema kuwa
kituo hicho cha Runinga maarufu hapa nchini (jina tunalo) kilitangaza
habari za kupotosha umma kuwa wakulima wa mpunga pawaga
wameandamana hadi ofisi ya Halmashauri ya wilaya Iringa kupinga
ushuru mkubwa wa mpunga jambo ambalo si kweli.
Alisema kuwa waliofanya maandamano
hayo hawakuwa wakulima bali wakuliwa wafanyabiashara wa mpunga
waliopo mjini Iringa kwa lengo la kuidanganya serikali kama ni
wakulima wakati si kweli.
Kwani alisema kuwa lengo la
wafanyabiashara hao ni kutaka kuendelea kuwanyonya wakulima na sio
vinginevyo na hivyo kuwataka wanahabari kuwa makini katika kuandika
habari na kuwa kabla ya kutangaza basi kufanya uchunguzi wa kina
ili kuwa na usahihi badala ya kutoa habari za kupotosha umma.
Dkt Ishengoma alisema kutokana na
maandamano hayo vyombo vya usalama mkoani hapa vimewahoji
wafanyabiashara hao na kukubali kudanganya umma kuwa wao ni wakulima
wa mpunga .
Hivyo alisema hatua ambazo
zimechukuliwa kwa wafanyabiashara hao ni pamoja na kutakiwa
kulipa ushuru na kuwa hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa
dhidi yao kwa tukio hilo.
Hata hivyo alisema kuwa hakuna
mkulima ambae amekuwa akitozwa ushuru kwa zao lao la mpunga na kuwa
ushuru uliopo ni kwa wafanyabiashara na si mkulima.
Pia mkuu huyo wa mkoa aliwataka
wakulima mkoani hapa kuwa makini na mbinu chafu za wafanyabiashara
katika uuzaji wa mazao yao ikiwa ni pamoja na kuzingatia vipimo
halali katika kuuza mazao badala ya kuuza mazao yao kwa matakwa ya
wanunuzi ya kutumia vipimo vya lumbesa ambavyo vimepigwa marufuku
mkoani Iringa.
HABARI NA FRANCIS GODWIN
0 comments:
Post a Comment