Mratibu msaidizi wa kudhibiti ukimwi mkoa wa Iringa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya kudhibiti ukimwi na matumizi ya ukimwi
naibu meya wa manispaa ya Iringa Gervas Ddaki akifungua mdahalo wa kudhibiti ukimwi na matumizi ya madawa ya kulevya
mmoja wa wanafunzi Neema Magoma akichangia mada katika mkutano huo
Halmashauri ya Manispaa ya Mkoa wa Iringa umeandaa mikakati thabiti ya namna ya kupambana na kuzuia maambukizi na matumizi ya madawa ya kulevya yanayozidi kuongezeka kwa kasi mkoani hapa.
Mwandishi wetu Denis Mlowe anaripoti kuwa hayo yamesemwa na Msaidizi wa Kudhibiti maambukizi ya virus vya ukimwi Gasper Nsanye wakati wa mdahalo ulioandaliwa na AMMICAL wa mpango wa majadiliano ya viongozi na wadau mbalimbali ulifanyika katika ukumbi wa hallfare na kuwashirikisha rika mbalimbali wakiwamo wanafunzi wa vyuo vikuu, sekondari na shule ya msingi na kufaidisha mkoa wa Iringa na wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala za Dar es Salaam.
Alisema kwamba mkoa wa Iringa umekumbwa na makundi matatu ambayo yamesaulika katika jamii kuhusiana na maambukizi ya ukimwi na na matumizi ya madawa ya kulevya na ndio chanzo cha kuenea kwa kasi kubwa katika manispaa na kuifanya kuwa ya kwanza kitaifa kwa maambukizi ya ukimwi.“Lengo la kufanya mdahalo huu ni juu ya athari za dawa za kulevya na ukimwi kuzuia na kudhibiti kabisa hadi kufikia hatua ya sufuri 3 katika kuenea kwa ukimwi, unyanyapaa na biashara ya madanguro na vijana wanaotumia madawa ya kulevya kufikia hatua ya sifuri 3” alisema Nsanye
Aidha alisema kwamba mkoa wa Iringa ni wa kwanza kitaifa ukiwa na asilimia 15.7 hivyo lengo pia ni kuweka mikakati ya namna ya kukabiliana na vvu na ukimwi ili kupunguza vifo kufikia sifuri na kusaidia makundi hayo matatu ambayo ni baishara ya ngono,wanaojidunga madawa ya kulevya na wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsi moja(ushoga).
Awali Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki alisema kwamba kwa sasa Iringa imeingiliwa na makundi hayo na ndio chanzo kikubwa cha kuenea kwa maambukizi katika manispaa na ni jukumu la kitu mwananchi kuweza kupambana na makundi haya kwa kuwapa elimu na kuweza kuwasaidia kuondokana na tabia hatarishi. “ Ni lazima tutokomeze haya makundi na jamii yatakiwa kutambua kwamba makundi haya yapo na yanasababisha maambukiz makubwa ya virus vya ukimwi katika mkoa wa Iringa” alisema Ndaki.
Naye mwenzeshaji Dr Jayson Mboya alisema kwamba kwa sasa watu milioni 33.3 wanaishi na virus vya ukimwi na wengi wao wako Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania yenye watu milioni 1.6 na chanzo kikubwa ni ngoni zembe zikiambatana na tabia hatarishi kama kujidunga madawa ya kulevya kwa kuazimana sindano, unywaji wa pombe kupita kiasi na wafungwa wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Alisema jamii yatakiwa kuelimishwa kwa kiasi kikubwa madhara na athari ya utumiaji wa madawa ya kulevya waweze kujiepusha na kutotumia kabisa aidha kuongezwa kwa vituo vya afya vitakavyohudumia waathirika wa madawa kulevya na vijana kujishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo michezo.
Chanzo: Francis Godwin
0 comments:
Post a Comment