Home » » IPC YAZIBA PENGO LILILOACHWA NA MAREHEMU DAUD MWAGOSI

IPC YAZIBA PENGO LILILOACHWA NA MAREHEMU DAUD MWAGOSI


mwenyekiti mteule  wa IPC  Frank Leonard (kushoto) na katibu mtendaji  wa IPC Francis Godwin kulia tukiteta jambo katika moja kati  ya vikao vyetu mwaka jana
Aliyekuwa mweka hazina wa IPC marehemu Vicky Macha
Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Marehemu Daud Mwangosi na  chini siku alipouwawa  kinyama
Klabu ya waandishi wa  habari mkoa wa  Iringa (IPC) leo imekamilisha  kuziba mapengo ya uongozi yaliyokuwemo ndani ya IPC  kufuatia  kifo cha aliyekuwa  mwenyekiti wake marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa tarehe 2/9/2012 Nyololo katika vurugu  za polisi na  Chadema, pia nafasi ya mweka hazima wake mkuu Vicky Macha aliyefariki  mwezi  wa 10/2012 pamoja na nafasi za  wajumbe  watatu  wakamati  ya utendaji .

katika  uchaguzi huo uliofanyika leo wakati  wa mkutano maalum wa uchaguzi  wa IPC  uliofanyika Hotel ya M.R mjini Iringa  msimamizi mkuu  wa uchaguzi huo Frederick Siwale  aliwataja  waliochaguliwa kuwa ni pamoja na aliyekuwa katibu mtendaji  wa IPC Frank Leonard aliyepata  kura  17 kati ya  kura 18 zilizopigwa katika nafasi hiyo ya uenyekiti  iliyokuwa  ikigombewa na mwanachama Zulfa Shomari aliyetangaza  kujitoa na kuomba  wajumbe  kumchagua Leonard kutokana na utendaji wake mzuri , wakati makamu mwenyekiti amepita  bila kupingwa Jackson Manga aliyepata  kura  zote 18 za  wajumbe  wa mkutano  huo ambao jumla ya  wanachama  hai  wa IPC ni 24  ila  waliofika  leo ni 18  wakati nafasi ya katibu mtendaji  wa IPC imechukuliwa na aliyekuwa naibu katibu mkuu wa IPC Francis Godwin aliyepata  kura  za ndio 16 huku  kura  2 zikimkataa .

Wengine  waliochaguliwa ni pamoja na mweka  hazina mkuu  wa IPC Janeth Matondo  aliyechukua  nafasi ya marehemu  Vicky Macha kwa kupata  kura  zote  za ndio 18  pamoja na mweka hazina msaidizi  Suleiman Boki  aliyepata  kura  zote 18 .

Wajumbe  watatu  waliochaguliwa ni  Hapy Matanji  aliyepata kura  (18) Swiga  Mwaisumbe (18 ) na Selina Ilunga(17).
Na Francis Godwin 

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa