Home » » HALI YA AFYA YA MBUNGE CHIKU ABWAO BADO SI NZURI , SOMA HAPA

HALI YA AFYA YA MBUNGE CHIKU ABWAO BADO SI NZURI , SOMA HAPA


 Mbunge  Abwao akiwa na  waziri mkuu Mizengo Pinda

Pamoja na  kuruhusiwa katika  Hospitali ya mkoa  wa Iringa ambako mbunge wa viti maalum mkoa  wa Iringa  kupitia  chama  cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Chiku Abwao alikokuwa akitibiwa bado hali  yake kiafya ni mbaya  .

Mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com umeelezwa kuwa  mbunge Abwao kwa  sasa amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa  ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi  baada ya  afya yake  kuendelea  kuteteleka  .

Jitihada  za kumtafuta  mbunge Abwao zinaendelea  ili  kujua afya yake zaidi  kutokana na tatizo hilo la uvimbe katika mguu  wake ambalo  linamsumbua .

Habari imeandika na Francis Godwin

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa