Home » » DC MUFINDI APIGA MARUFUKU WALIMU KUFUKUZA WANAFUNZI KWA MICHANGO....

DC MUFINDI APIGA MARUFUKU WALIMU KUFUKUZA WANAFUNZI KWA MICHANGO....


MKUU wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Evarista Kalalu  (pichani)apiga marufuku walimu kuwafukuza wanafunzi kwa kukosa kulipa michango mbali mbali na kutaka walimu kuwabana wazazi sio kuwarudisha nyumbani watoto.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa agizo hilo leo wakati akifungua kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri
hiyo.

Alisema kuwa suala la kuwabana wazazi wadiolipa michango linapaswa kufanywa na watendaji wa kata na vijiji badala ya kuwaachia walimu wakuu pekee .

Pia awataka watendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa ushirikiano zaidi ili kuchochoa kasi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Amesema  iwapo watendaji wataendelea kufanya kazi bila ushirikiano kasi ya maendeleo katika wilaya hiyo itaendelea kuyumba na watendaji hao watakuwa wakiwakosea wananchi ambao wanategemea huduma bora Kutoka kwa Halmashauri yao.

Aidha mkuu huyo wa wilaya ameagiza viongozi wa wilaya hiyo kuwabana wazazi wote ambao wanashindwa kuwapeleka watoto shule kwa kisingizio cha kukosa fedha.

Kwani alisema kuwa lazima viongozi kufanya utafiti wa kina kwa kuwatembelea wanafunzi ambao wanapaswa kwenda shule na hawajapelekwa ili kujua tatizo ni nini na Kama mzazi ana mifugo basi abanwe ili kuuza mifugo kwa ajili ya kusomesha mtoto sekondari badala ya kusingizia kipato wakati mifugo ipo.

Alisema kuwa kwa wazazi wasio na uwezo kabisa basi serikali itachukua hatua ya kusomesha watoto hao.

Wakati huo huo mkuu wa wilaya huyo ameagiza madiwani kwa kushirikiana na watendaji wa kata kuwasilisha taarifa za utendaji kazi katika kata zao ili kuongeza kasi ya utendaji zaidi.

Kalalu alisema kuwa tayari waziri mkuu ametoa agizo hilo kwa madiwani wote nchini kufanya hivyo na kuwa lazima agizo hilo kuanza kutekelezwa kwa kasi zaidi.

Akielezea Suala la matumizi ya pembejeo za ruzuku mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa katika kujiandaa kwa kilimo mwaka 2013/2014 alisema kuwa mikopo itatolewa kupitia vyama vya ushirika hivyo lazima viongozi kuanza kuhimiza wananchi kujiunga na vyama vya ushirika.

 Alisema kuwa iwapo wananchi hawataandaliwa kujiunga na vyama hivyo itakuwa ni vigumu kuweza kutekeleza mpango huo ,huku akiwataka watendaji kusimamia vema utaratibu wa sasa wa vocha za ruzuku ili kuhakikisha. Vocha zote zinatumika kwa wakulima badala ya kurudishwa Halmashauri wakati wakulima wakiwa bado wanahitaji.

 Kwa Upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Limbaksye Shimwela alisema kuwa katika kuongeza kasi ya uwajibikaji kwa watendaji wa Halmashauri hiyo ofisi yake imeanzisha utaratibu wa kuulizwa Maswali ya papo kwa papo kwa mkurugenzi katika vikao vya madiwani.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa