Ndugu zangu,
Najiandaa na salamu za Mwaka Mpya kwa ' Wanakijiji wangu' wa Mjengwablog, Kwanza Jamii na marafiki zangu wa FB.
Imekuwa ni utamaduni niliojiwekea tangu mwaka 2006 nilipoanzisha Mjengwablog. Na salamu za Mwaka Mpya hutolewa mara moja tu kila mwaka, Desemba 31, ni kesho.
Ni salamu za mwisho kwa mwaka na zenye kutuvusha kwenda kwenye mwaka mpya. Ni tukio muhimu sana.
Najiandaa vipi?
Ni kwa kutembea kwa miguu peke yangu japo saa nzima huku nikitafakari. Kisha nitahitaji kula saladi ya matunda na vikombe vya chai ya rangi bila sukari kabla sijaanza kuyaandika niliyoyafikiri.
Na hata kwa maandalizi hayo haimaanishi kuwa salamu haziwezi kukosa mapungufu, maana, ni kwa vile zinaandikwa na mwanadamu asiyekamilika.
Muhimu ni kutambua, kuwa kwa kila jambo unalotaka kutenda, basi, jitahidi kufanya maandalizi. Na maanandalizi yasifanywe siku ya tukio lenyewe.
Wahenga walisema; ng'ombe hanenepi siku ya mnada!
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0 comments:
Post a Comment