Bw. NICHOLAUS PIUS MWINUKA ambaye ni Mmoja kati ya walemavu wawili waliopatiwa msaada wa baiskeli kutoka kwa mbunge Deo Filikunjombe .
Jina la mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe limeendelea kutumiwa vibaya na wananchi wa mkoa wa Njombe ambao wameanza kulitumia jina hilo kufanyia vitendo vya utapeli mtandao huu umebaini.
Imedaiwa kuwa matapeli hao wamekuwa wakitumia jina la mbunge huyo Deo Haule Filikunjombe kwa kupigia watu simu na kuomba kutumiwa fedha jambo ambalo ni sawa na utapeli wa kutupwa .
Katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com unaonyesha kuwa baadhi ya watu tayari wamekwisha lizwa na utapeli huo ambapo matapeli hao wamekuwa wakijitambulisha kuwa wao ni Deo Haule Filikunjombe japo si kweli.
Hadi sasa tayari watu kadhaa wamelizwa kupitia jina la mbunge huyo na kuwa wapo waliosajili namba zao kama Deo Haule kumbe ni matepeli na mmoja kati ya walionusurika kutapeliwa ni pamoja na mkurugenzi wa kituo cha radio Njombe ambae alionyesha kushitukia utapeli huo .
Kwa upande wake mbunge Filikunjombe amewataka wananchi kuwa makini na utapeli huo na kuwa hana kawaida ya kutumia mtu kuazima pesa na kuwataka wananchi wasikubali kuamini mazungmzo ya kwenye simu ambayo hutumiwa na matapeli hao .
Filikunjombe pia amewapa pole wale wote waliotapeliwa na matapeli hao na kuwataka kuwa makini na utapeli huo .
0 comments:
Post a Comment