Wanahabari wakiwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za afya
HOSPITALI ya mkoa wa Iringa ilivyojipanga kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa damu salama kupitia mpango wa Taifa wa damu salama.
na Francis Godwin Iringa
Ikumbukwe kuwa damu ni moja kati ya mahitaji muhimu katika mwili wa binadamu awaye yeyote ili aweze kuishi ni lazima kuwa na damu ya kutosha mwilini mwaka.
Hospitali na vituo vya afya vya umma na binafsi ila bado uelewa wa baadhi ya wananchi katika kujitolea kutoa damu limekuwa ni tatizo kubwa kutokana na jamii kutokuwa na utamaduni wa kufika katika banki za damu kwa ajili ya kutoa mchango wa damu.
Tayari serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii imekwisha toa mwongozo wa damu salama kama njia ya kujipanga kuboresha huduma hiyo .
Lengo la kutoa mwongozo kwenye uundwaji wa kupangwa vizuri huduma kuongezewa damu, sambamba na Azimio la Afya Duniani Bunge WHA 28.72 (iliyopitishwa Mei 19, 1975) kwamba linataka nchi wanachama wote wa kuendeleza uratibu wa kuongezewa damu ni huduma ya msingi na hiari
Pia kupangwa vizuri Damu (BTS) ni sehemu muhimu ya mfumo wowote wa afya kujifungua ili kufanikisha mpango huo mkakati madhubuti kwa ajili ya Usalama wa Damu inahitajika
Kutoka 2003 hadi 2007, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Marekani imefanya ukarabati wa vituo 7 vya kanda ambapo shughuli za mpango wa damu salama umetekelezwa.
Vituo hivi kanda (ZC) ambayo ni ya kijiografia aitwaye ni Ziwa (Mwanza), Kaskazini (Moshi), Magharibi (Tabora), Mashariki (Tabora), Kusini (Mtwara), na nyanda za juu Kusini (Mbeya) na Zanzibar.
Meneja wa maabara ya mkoa wa Iringa Kimea Myefu amesema kuwa katika kutekeleza mpango huo na kuona kuwa Hospitali ya mkoa wa Iringa haipungukiwi na akiba ya damu salama katika benki yake imekuwa na mpango maalum wa kupata damu salama kwa kutenga bajeti maalum ya kusafirisha damu kutoka Mbeya .
Myefu amesema kuwa kutokana na mpango makakati huo wa kutenga bajeti ya kusafirisha damu kwa kiasi tatizo la damu katika benki ya damu salama Hospitali ya mkoa kutokuwa tatizo sana.
Hata hivyo amesema kuwa mwamuko kwa jamii katika kujitolea damu katika mkoa wa Iringa umekuwa mkubwa zaidi ukilinganisha na miaka ya nyuma kabla ya kuanzishwa mpango huo wa damu salama .
Myefu amesema kuwa idadi kubwa ya wananchi wanaofika kuchangia damu tayari wana elimu juu ya mpango huo na wanajua afya zao ila wale wasiojua afya zao ndio wamekuwa nyuma kujitokeza kuchangia damu.
“Kwa sasa idadi kubwa ya watu wanaojitokeza kuchangia damu zao wamekuwa wakichangia damu ila idadi ndogo hasa wale ambao ni wageni kabisa katika kuchangia damu ndio ambao wamekuwa wakiondoka bila kuchangia damu kutokana na kutokuwa na uhakika wa afya zao”amesema Myefu
Kuwa imeendelea kutolewa na wananchi wengi wamekuwa wakijitokeza kuchangia damu na kati ya watu 10 wanaofika kutoa damu ni wawili ama mmoja pekee ndie ambae amekuwa akirudi pasipo kuchangia damu kutokana na matatizo ya kiafya.
Aidha amesema kuwa kuna haja ya jamii kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara ili pale ambapo mchango wao wa damu utahitajika basi kuweza kufika katika katika benki za damu na kuchangia damu.
Akielezea kuhusu utaratibu wa mchangiaji wa damu Myefu amesema kuwa kwanza ni lazima kupimwa H.I.V , homa ya ini , magonjwa ya zinaa kama kaswende na mengine ,kiasi cha damu alichonacho mchangiaji pamoja na matatizo ya presha ,Kwani amesema kitaalam mwenye kuchangia damu ni lazima awe na uzito wa kuanzia kilo 50 na kuendelea.
Akielezea kuhusu mahitaji ya kawaida ya damu katika Hospitali hiyo ya mkoa kwa siku kuwa ni uniti 8 na kuendelea wakati akiba ya damu iliyopo kwa sasa ni uniti 25 ambacho bado kidogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya siku.
Hivyo ameiomba jamii kujenga utamaduni wa kujitolea kuchangia damu mara kwa mara ili kuboresha zaidi huduma hiyo .
Myefu amesema kuwa baadhi ya wananchi wanaofika kuchangia damu kwa ajili ya wagonjwa wao wamekuwa wakiamini kuwa damu wanayochangia ni kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa wao jambo ambalo halina ukweli wowote.
“Kimsingi kama kuna mgonjwa anahitaji damu na ndugu wakajitolea kuchangia damu damu hiyo haiwezi kutumika kwa wakati huo kwa ajili ya mgonjwa wake isipokuwa atapewa damu nyingine ambayo imetoka kituo cha damu salama cha kanda kilichopo mkoa wa Mbeya na si vinginevyo”
Kwani amesema kuwa damu inayochangiwa na katika Hospitali ya mkoa haitumiki hadi ipelekwe katika kituo cha kanda kwa ajili ya kuihakiki ubora wake.
Pia amesema kuwa damu imekuwa na matumizi makubwa hasa pale inapotokea ajali na majeruhi kufikishwa katika hospitali hiyo.
Myefu amesema kwa mchangiaji wa damu hakuna malipo yoyote zaidi ya kupongeza kwa neon la ahsante na kuwa hakuna biashara ya damu inayofanyika katika Hospitali hiyo.
Wakati Hospitali hiyo ya mkoa wa Iringa ikiwa na mkakati huo wa kuboresha zaidi mpango huo wa damu salama uchunguzi uliofanywa na wanahabari wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) wanaopatiwa mafunzo ya uandishi wa habari za afya chini ya ufadhili wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umebaini kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya mpango huo huku wengi wao wakitaka kulipwa wanapokwenda kutoa damu.
Sara Kalinga mkazi wa Kihesa Iringa amesema kuwa kwa upande wake amekuwa gizani juu ya mpango huo na kuwa kuna haja ya elimu zaidi kuendelea kutolewa ili wananchi waweze kujenga utamaduni wa kujitolea damu ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu salama katika benki ya damu.
Huku Joseph Ndelwa akidai kuwa serikali inapaswa kuweka utaratibu wa kuwalipa fedha wananchi wanaojitolea damu ili kuhamasisha zaidi wananchi kuchangia mpango huo wa damu salama.
www.francisgodwin.blogspot.com /0754026299
0 comments:
Post a Comment