Home » » WAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA VIRUSI VYA UKIMWI

WAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA VIRUSI VYA UKIMWI

Mwandishi wetu, Iringa Yetu

KATIKA hali isiyo ya kawaida,Balozi wa Marekani nchini ALFONSO LENHARDT  amejikuta akishindwa kuamini anachosikia baada baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wanaoishi na virusi vya ukimwi kumshukuru Mungu kwa kuwapatia virusi hivyo.

Wananchi hao walitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Balozi huyo wa Marekani kuzindua rasmi Kituo cha Afya cha Alamano kinachoendeshwa na Watawa wa Kanisa Katoliki, kilichokarabatiwa kwa msaada wa wananchi wa Marekani,kitu ambacho hutoa huduma mbalimbali kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Manispaa ya Iringa.

Baadhi ya wananchi hao ni Eliza Muhumba na Bwana Wito Chavala ambao wamedai kuwa huenda Mungu alikuwa na maksudi yake kuwafanya wapate virusi vya ukimwi kwa maelezo kuwa baada ya kupata virusi hivyo,maisha yao kiafya na kiuchumi yameimarika zaidi ikilinganishwa na wakati hawajaambukizwa kutokana na huduma mbalimbali ikiwemo za tiba na mikopo midogo midogo wanayopata kutoka Alamano Centre

Kufuatia kauli hizo,Balozi wa Marekani Alfonso Lenhardt alileza kuguswa nazo na kusema kuwa kuimarisha afya za watanzania ni moja ya vipaumbele vya ubalozi wa Marekani nchini Tanzania

Kwa msaada wa Marekani,Alamano Centre mpaka sasa inahudumia watu watu wanaoishi na virusi vya ukimwi karibu 4,000 ambapo 2000 wanapata huduma na misaada mbalimbali na 1800 wanapata tiba ya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi.

Blogzamikoa

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa