Home » » MWANDISHI WA HABARI TBC AIBIWA KAMERA NA KOMPYUTA PAKATO(LAPTOP) CHUMBANI KWAKE.

MWANDISHI WA HABARI TBC AIBIWA KAMERA NA KOMPYUTA PAKATO(LAPTOP) CHUMBANI KWAKE.




Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1)  Ndugu Hosea Cheyo.





Habari na Ezekiel Kamanga, Iringa.


Mwandishi wa habari wa wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC1 mkoani Mbeya Bwana Hosea Cheyo ameibiwa Kamera na kompyuta pakato yaani Laptop vyenye thamani ya shilingi 1,800,000 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Happy Lodge iliyopo jirani na kituo kikuu cha mabasi cha Iringa, Oktoba 2 mwaka huu majira ya 1:30 asubuhi.





Mwandishi wa habari huyo alikuwa mkoani Iringa kuhudhuria semina ya waandishi wa habri wa Nyanda za Juu Kusini inayohusu mchakato wa Katiba iliyoandaliwa na Baraza la Habari nchini MCT kuanzia Oktoba 22 mwaka huu hadi Oktoba 24 mwaka huu katika Ukumbi wa Maktaba uliopo Manispaa ya Iringa.





Bwana Cheyo amesema Oktoba 24 asubuhi alipokuwa kuoga alifunga mlango kwa ufunguo na aliporudi alishangaa kuona vifaa vyake havipo, hali iliyomfanya kutoa taarifa kwa mhudumu wa nyumba hito ya kulala wageni na hakuwa na maelezo ya kutosha.





Mwandishi huyo amedai kuwa mbinu iliyotumika kufungua mlango wake ni kutumia ufunguo bandia na kisha wezi hao kuingia kiurahisichumbani humo na kuondoka na vifaa vyake vya kazi.





Aidha Bwana Cheyoaliotoa taarifa Kituo cha Polisi Mkoani humo na kufunguliwa jalada lenye namba IR/RB/6350/012 na kwamba Jeshi la polisi linamshikilia mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa mahojiano zaidi.





Hata hivyo ilibidi Bwana Cheyo kushindwa kuendelea na semina  ili kushughulikia tatizo hilo, huku Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoani Mbeya Bwana Christopher Nyenyembe, amempa pole  mwandishi huyo wa TBC kwa kuibiwa nyaraka muhimu na kuwataka wamiliki wa nyumba za wageni kukomesha vitendo vya wizi vinavyofanywa na wahudumu wao.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa