Home » » MGOGORO WA MUDA MREFU WA MBOMIPA WAMALIZIKA

MGOGORO WA MUDA MREFU WA MBOMIPA WAMALIZIKA



Mwandishi wetu, Iringa Yetu
MGOGORO uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili katika Jumuiya ya Matumizi Bora Malihai Tarafa za Idodi na Pawaga (MBOMIPA) wilaya ya Iringa hatimaye umepatiwa ufumbuzi na kumalizika.
Vijiji 21 vinavyounda Jumuiya hiyo vilikuwa katika mgogoro mkubwa wa namna ya kugawana mapato yanayotokana na vyanzo vyake lakini katika Mkutano kati ya Mkuu wa wilaya ya Iringa,wenyeviti wa vijiji hivyo 21 na Shirika la hifadhi ya wanyamapori –WCS, mgogoro huo ukapatiwa ufumbuzi.

Vijiji hivyo 21 ni vijiji vinavypakana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha na baadhi yake vilitoa ardhi kwa ajili ya hifadhi ya jamii na vimekuwa vikipata hadi Sh.milioni 140 kwa mwaka kutokana na utalii wa picha na uwindaji wa kienyeji na uwindaji wa kitalii.

Mkuu huyo wa wilaya Dkt.Reticia Warioba anasema ni wakati sasa wa kusonge mbele kwa jumuiya hiyo baada ya kumalizika kwa mgogogoro huo.

Awali Mkurugenzi wa WCS aliwaomba wajumbe wa mkutano hao kujali maslahi ya Jumuiya kwa kuumaliza mgogoro huo baada ya hali ndani ya ukumbi kuwa tete huku baadhi ya wenyeviti wa vijiji wakitishia kwenda mahakamani

Kabla ya mgogoro huo kumalizika, vijiji vinane vilikuwa vimesusa mgawo wa mapato ya mbomipa vikipinga kugawana sawa ni vijiji ambavyo ama vilitoa ardhi kidogo ya uhifadhi au havikutoa kabisa.
Blogzamikoa


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa