Home » » TAHARIRI: SERIKALI ITOE ULINZI KWA MWANDISHI FRANCIS GODWIN

TAHARIRI: SERIKALI ITOE ULINZI KWA MWANDISHI FRANCIS GODWIN

Francis Godwin akiwa na mke wako muda mfupi baada ya kupanda basi kuelekea mafichoni

--------------------------------------
 Mwandishi wa habari na mwanaharakati wa kutetea haki za wanyonge mkoani Iringa Franics Godwin jana ameandika waraka akielezea hofu yake ya kuuawa na jeshi la polisi kwa kile anachokisema ni kuwa na ushahidi wa tukio zima la kuuawa kwa mwandishi wa Channel 10, Daud Mwangosi.
Francis Godwin mbali na kufanya kazi kwa karibu na marehemu Mwangosi pia alikuwa shemeji wa marehemu ambaye alikuwa mwanaharakati wa kweli katika kutetea wanyonge.
Katika waraka huo Godwin amesisitiza uamuzi wake wa kuukimbia mkoa wa Iringa na kwenda mafichoni akihofia usalama wake juu ya tishio la kuaawa.
Kwa namna yeyote ile madai na uamuzi wa mwandishi huyo yanatakiwa kufanyiwa kazi na serikali ili kutengua njama ambazo zinaonekana kupangwa kutekelezwa na watu wasio na nia njema na wanahabari.

Katika kipindi hiki kigumu ambacho jeshi la polisi linajaribu kutafuta mahala pakuficha maovu yao hasa kwa kuongezeka kwa matukio ya kutumia nguvu na silaha za moto dhidi ya raia inaweza kufanya lolote ili kujisafisha.
Watu kama Francis na wengine wanaweza kuwa chambo na kutolewa kafara kwa njia yeyote ile, kwani tayari jeshi la polisi wameanza kumuwinda kijana huyu na wengine na kumtaka kuwa shahidi katika tukio hilo badala ya kuwasaka wauwaji ambao walionekana moja kwa moja hata katika picha zilizopigwa siku ya tukio.
Ni dhahiri polisi inatapatapa kutafuta njia ya kujinasua na kashfa hii lakini awamu hii kama haki itatendeka hakuna atakayepona.
Lengo la polisi ni kumshinikiza kijana huyo na wengine ambao walikuwa katika eneo hilo siku ya tukio kutoa ushuhuda wa uongo ili kupoteza ukweli kamili, polisi acheni njia hizo za kizamani, ukitaka kuuzima moshi zima moto chini.
Serikali inapaswa kutoa ulinzi kwa mwandishi huyu na wengine wote waliokatika hatari ya kupoteza maisha yao kwa kutetea na kusimamia ukweli kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla
Blogzamikoa

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa