Home » » KAMATI YA UCHUNGUZI KIFO CHA MWANGOSI WAIBIWA VITENDEA KAZI IRINGA

KAMATI YA UCHUNGUZI KIFO CHA MWANGOSI WAIBIWA VITENDEA KAZI IRINGA


Marehemu Daudi Mwangosi.
Ikiwa ni siku moja tu baada ya kufikishwa Mahakamani kwa askari polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya mwandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi, Kamanda wa polisi Iringa Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa wizi uliofanywa kwa kamati iliyoundwa kuchunguza kifo hicho.
Namnukuu akisema “ni kweli wamefanyiwa uhalifu hotelini kwao wakiwa hawapo, imeibwa Ipad pamoja na shilingi laki tisa, bado tunamtafuta mwizi ambae bado hajajulikana”

Juzi September 12 ndio askari anaetuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na baadae kurudishwa mahabusu.

Imekua ngumu kuwapata wahusika lakini DJ SEK BLOG inaendelea kuwatafuta ili kujua mazingira ya wizi na kama kuna ushahidi wowote uliopotea pamoja na mambo mengine.
Chanzo: Dj sek blog 

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa