Home » » MUFINDI WAANZA KUTUMIA AINA MPYA YA MBOLEA

MUFINDI WAANZA KUTUMIA AINA MPYA YA MBOLEA


Mwandishi wetu, Mufindi-Iringa Yetu
SERIKALI imetoa tamko kuhusu mpango wake wa kusambaza pembejeo za ruzuku pamoja na aina nyingine ya mbolea ya Minjingu badala ya mboea ya DAP ambayo itatolewa kwa wakulima katika msimu ujao wa kilimo.

Pamoja na aina hiyo ya mbolea pia wakulima watapata ruzuku ya mbegu za alizeti na mtama itakatotumika kwa maeneo ambayo kuna ukame ili kuongeza mazao ya chakula.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mpango wa hiyo, Afisa kilimo na ushirika Edna Kaduma, ameeleza jinsi gani pembejeo hizo zitawafikia wakulima.

Mkuu wa wilaya ya Mufindi ametoa ushauri kwa viongozi wa Kata na Tarafa kuwaelimisha wakulima ili waweze kutumia aina hiyo ya mbolea.


Kutokana na mabadiliko hayo ya pembejeo mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini Mendarad Kigola ameonesha mashaka juu ya mabadiliko hayo na kwamba ushauri unahitajika ili kutowayumbisha wakulima.

Blogzamikoa

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa