Home » » WALI WA SHEREHE WAUA MMOJA, 40 WALAZWA IRINGA

WALI WA SHEREHE WAUA MMOJA, 40 WALAZWA IRINGA


Mmoja wa waathirika wa chakula hicho akiwa hospitalini.
Mganga Mfawidhi wa kituo cha Ipogolo ambaye jina lake halikupatikana.
Wagonjwa wengine walioathirika na chakula hicho wakiwa wodini.
MTU mmoja mkazi  wa kijiji cha Ibofye wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa aitwaye Wagila Nyaupumba, amefariki dunia na  wengine zaidi ya 40  wamelazwa  katika  hospitali  mbalimbali za mkoa  wa  Iringa  kikiwemo  kituo cha  afya  cha Ipogolo  na Hospital ya Rufaa ya Mkoa  wa Iringa baada ya  kula wali  na kunywa  togwa  vinavyosadikika   kuwa na sumu katika  shehere ya  kutoa mahari.
Tukio hilo lilitokea  juzi  Jumamosi  baada ya  mkazi  wa kijiji hicho,  James Ngaile,  kuandaa chakula na kinywaji hicho  kwa  kwa ajili ya  sherehe ya  kuoza  binti  yake.
Habari zilizopatikana zinasema baada ya kula chakula  hicho na kufika nyumbani usiku, waathirika walianza kuharisha damu na baadaye kukimbizwa hospitali ambapo marehemu alifariki na wengine hali zao zinaendelea vizuri.
Kamanda  wa  Polisi  wa Mkoa  wa Iringa, Michael Kamhanda,  alipoulizwa na mwandishi  wa habari  hizi kwa njia ya simu jana kuhusu tukio  hilo alisema bado halijafika  ofisini kwake na kuwa  pindi  litakapomfikia atalitolea  ufafanuzi.
Na  Francis  Godwin, Iringa

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa