Na Francis Godwin-Iringa
Wakati kesho mei 3
ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani
,wanahabari mkoa wa Iringa wamepanga kufanya maandamano makubwa kwa
ajili ya kuadhimisha siku hiyo pamoja na kumweka kiti moto mbunge wa
jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya wananchi wengi
kumlalamikia mbunge huyo .
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa
habari mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi aliyasema hayo leo wakati
akizunguza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya siku hiyo ya
Uhuru wa Vyombo duniani .
Alisema kuwa mdahalo huu katika ya
wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini na mbunge huyo wa jimbo la Iringa
mjini Mchungaji Peter Msigwa utafanyika katika ukumbi wa Highlands
ukumbi uliopo katikati ya mji Iringa kutoa nafasi kwa wananchi wote
kufika.
Hata hivyo alisema kuwa mdahalo huo ulipangwa
kuwahusisha pia wabunge wa CCM akiwemo mbunge wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM)
ambao wameonyesha kuwa na uzuru katika siku hiyo .
Alisema kuwa
wakati mbunge Kabati akiomba kutofika kutokana na kuwa katika vikao
jijini Dar es Salaam mbunge Filikunjombe kwa siku hiyo atakuwa nje ya
nchi hivyo kufika kwao itakuwa vigumu.
Mwangosi alisema sherehe
hizo za siku ya uhuru wa vyombo vya habari zitahusisha wanahabari wote
bila kujali ni wanachama wa IPC ama si wanachama.
katika hatua
nyingine Mwangosi alisema kuwa IPC inasikitishwa na vitendo vitisho
vinavyotolewa na wanafunzi wa chuo cha elimu Mkwawa Iringa kwa
wanahabari wa vyombo mbali mbali wanaofika kusikiliza madai yao katika
migomo mbali mbali.
Alisema kuwa wanafunzi hao wamekuwa na tabia
ya kuwaita wanahabari wakati wa migomo yao na mara baada ya kufika na
kuripoti wamekuwa wakiwatishia kuwavunjia vifaa vyao vya kazi kwa madai
kuwa kwanini wanahabari hao wamewafuata watuhumiwa katika madai hayo na
kuwahoji kinyume na wao wanavyotaka kuzungumza wao pekee.
Mwangosi
alisema kuwa tayari wanahabari hao wamepata kutoa vitisho kwa mwandishi
wa TBC Iringa , Chanel Ten, gazeti la Mtanania ,Habari leo , Radio
Ebony Fm ,Radio Country Fm na wanahabari wengine wengi .
Hivyo
amesema kuwa iwapo wanafunzi hao wataendelea na tabia hiyo wanahabari
hawatakuwa tayari kwenda kuwasikiliza pale wanapohitaji uwepo wa vyombo
vya habari katika mambo yao.
Kwa upande wake katibu wa IPC Frank
Leonard alisema kuwa mbali ya kumweka mbunge Msigwa pia wanahabari hao
watashiriki katika usafi Hospitali ya mkoa wa Iringa pamoja na shughuli
nyingine za kijamii mjini Iringa.

0 comments:
Post a Comment