Na Francis Godwin Mzee wa matukio daima Blog- IRINGA
MBUNGE wa jimbo la Mufindi kusini Mendrady Kigola amcharukia waziri wa ujenzi John Magufuli mbele ya waziri wa maliasili na utalii Ezekiel Maige kuwa Magufuli ametelekeza barabara za jimbo la Mufindi na kumteka mwaka 2013 kabla ya uchaguzi mkuu barabara hizo ziwe zimetengenezwa.
Mbunge Kigola aliyasema hayo Leo katika kijiji cha Kibengu kilichopo jimbo la Mufindi kasikazini baada ya kumwakilisha mbunge wa jimbo hilo Mahamudu Mgimwa ambaye hakuwepo katika ziara hiyo.
Alisema kuwa hali ya barabara katika wilaya ya Mufindi ni mbovu kupita kiasi wakati wilaya nyingine nchini barabara ni nzuri zaidi.
Hivyo alimtaka waziri Maige ambaye ameshuhudia ubovu wa barabara hizo za wilaya ya Mufindi amepata kuzishuhudia na kuonja adha ya kero hiyo ya barabara kwa kusafiri zaidi masaa Matatu sehemu yenye umbali wa kilomita 70 wakati akitoka mjini Mafinga kuelekea katika kijiji hicho kutokana na barabara kuharibika zaidi.
Katika hatua nyingine mbunge Kigolla alimgeukia waziri Maige na kudai kuwa kuwa anashangazwa na wizara ya maliasili na utalii inayoongozwa na waziri Maige kuendelea kuvamia maeneo ya wananchi na kutaka wizara hiyo kuheshimu ardhi ya wananchi kwa kuacha uvamizi
Alisema kuwa miaka zaidi ya 1976 walikubaliana na misitu Sao Hill kuwa maeneo ya misitu na maeneo ya shughuli za wananchi kuonyeshwa ila sasa wizara hiyo ya maliasili imeendelea kuvamia makazi ya wananchi kwa kutaka watoke jambo ambalo yeye Kama mbunge na mbunge mwenzake wa jimbo hilo la Mufindi Kaskazini Mahamudu Mgimwa hawatakubali uvamizi huo.
Alisema kuwa wizara ya maliasili na utalii Ndio imekuwa ikiongoza kwa kufanya uvamizi wa ardhi ya wananchi katika maeneo ya wilaya ya Mufindi.
Mbunge Kigola alisema kuwa kila Mara serikali imekuwa ikiwataka waanchi kutunza ardhi yao bila kuitoa kwa wageni ila bado serikali imekuwa ikifika na kupora ardhi kwa nguvu.
Hata hivyo alisema kuwa maeneo ambayo wananchi hao wanaomba kupewa ni kutaka kuyatumia kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira kwa kuyafanya kuwa maeneo ya ardhi oevu.
Kwa upande wake mwekezaji Tekeleza Mwachang'a ambaye amewekeza katika vijiji zaidi ya 13 vya wilaya ya Mufindi ila bado amekuwa akikosa ardhi zaidi na kila anapoomba ardhi hukosa.
Sevelin Kilyenyi alisema kuwa wananchi wa eneo hilo ndio wamatunza chanzo cha maji cha Mtitu na Kihanzi ambavyo ni moja Kati ya vyanzo vikubwa vinavyowezesha Taifa kupata umeme wa uhakika.
Kuhusu suala la uvamizi alisema kuwa kijiji hicho hakijavamia ardhi kutokana na kuanzishwa zaidi ya mwaka 1976 na kwa kipindi hicho wao wamekuwa wakigawa ardhi kwa hifadhi ya misitu ya Saohill ila wanashangazwa sasa kuitwa wavamizi wa makazi yao.
Huku mzee Ignasi Msungu na paroko wa kanisa la Romani Katoriki Usokama Vicenti Mwagala walisema kuwa hawapendezwi na hatua ya serikali kuendelea kuwanyanyasa wananchi katika ardhi yao ambao imetolewa na Mungu ila mipaka imewekwa na binadamu.
Paroko Mwagala aliitaka serikali kuwa makini zaidi na kuwa suala la kusababisha wananchi wa Usokami Mufindi na kuwapeleka Kilimanjaro ni suala linalopaswa kufanyika mwishoni Kabisa .
Kwani alisema suala la serikali kutaka Sao hill Ndio iendelee Kupanda miti katika eneo hilo si maamuzi sahihi na kuwa hata wananchi wanaweza Kupanda miti kwa ajili ya uchumi wa Taifa bila kuwafukuza katika maeneo yao.
Kwa upande wake Waziri wa maliasili ma utalii Ezekiel Maige aliwataka wananchi hao kuheshimu sheria kwa kuvamia maeneo bila utaratibu na Kuahidi suala Lao kutafutiwa ufumbuzi kwa kutuma wataalam ambao watafika na kuona uwezekano wa kuwaachia ama kuendeleza eneo hilo.
Alisema kuwa lengo la serikali sio kupokonya maeneo ya wananchi Ila kuendeleza maeneo nyeti kwa rasilimali ya Taifa kwa ajili ya kusaidia ukuaji wa uchumi wa Taifa .
Waziri Maige alisema kuwa kwa maeneo yaliyopo katika hifadhi lazima wizara yake kufanya makubaliano na wahusika waliopanda miti katika maeneo ya hifadhi ili kuweza kuitunza na baada ya miti hiyo kukomaa basi wavune na kuachia ardhi hiyo kwa shughuli Za hifadhi.
Alisema kuwa mkoa wa Iringa kwa sasa baada ya kumegwa wilaya za Njombe ,Ludewa na Makete na kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Njombe ,makusanyo yake yanategemea uwepo wa msitu wa Sao Hill ambao unauingizia mkoa wa Iringa mapato ya zaidi ya asilimia 40.
Hivyo aliwataka wabunge wa majimbo ya wilaya ya Mufindi kulitazama suala hilo kwa upana zaidi Kwani iwapo ardhi itatolewa kiholela kuna uwezekano wa kuja kutokea matatizo kwa Taifa.
" Mimi niwaombe sasa waheshimiwa wabunge Kigola na Mgimwa mnapo simama kuwatetea wananchi juu ya ardhi lengeni kwenye hoja hiyo ya kuomba ardhi pekee sio Kwenda mbali zaidi kwa kutoa majibu na mapendekezo ya maombi hayo jambo ambalo ni sawa na kuwaziba midomo wananchi"
Kwani alisema kuwa serikali ina uwezo wa kutoa ardhi kwa wananchi popote ila uamuzi wa wananchi hao kutaka kupewa ardhi katika shamba la Taifa la Sao Hill ambalo ni Mali ya watanzania wote ni jambo lisilo wezekana ila wananchi hao wanaweza kuanza mchakato wa kudai ardhi kwa kuanza kupokonya ardhi ya wawekezaji wa kigeni waliofika kununua ardhi yao na sasa kuwaingiza katika uhaba mkubwa wa ardhi.
Japo alisema serikali haitapokonya miti iliyopandwa na wawekezaji hao katika ardhi hiyo waliyopewa na badala yake kuwaacha hadi wavune.
Waziri Maige alisema kuwa anashangazwa na hatua ya wananchi hao wa Kibengu kugawa ardhi kwa wawekezaji wakubwa ikiwemo kampuni za Green Resource,Gilanjo na Southern Highland Plantation pamoja na watu binafsi ambao ni wageni na maeneo hayo.
Aidha waziri Maige alisema kuwa tume yake itakayoundwa kuchunguza suala hilo la mgogoro wa ardhi katika eneo ndio itatoa uamuzi wa mwisho wa nini kifanyike kwa ajili ya mgogoro huo.
Katika hatua nyingine Waziri Maige alisema kuwa wizara yake imeanzisha utaratibu wa kuwawezesha wananchi wanaopanda miti kupata fedha za kutunza miti hadi pale itakapotakiwa kuvunwa .
Kuwa serikali imeanzishwa mfuko huo wa wananchi kutunza miti Yao kwa miaka japo 20 ili miti inayovunwa kuwa tayari kwa mavuno badala ya wananchi kuvuna miti michanga
kuhusu suala la barabara Maige alisema kuwa maombi ya mbunge Kigola kwa waziri Magufuli kuhusu ubovu wa barabara za wilaya ya Mufindi atayafikisha ili ikiwezekano waziri huyo kufanya utaratibu wa Kutembelea barabara hizo.
Wakati huo huo wananchi waliokuwa katika mkutano huo wa waziri Maige walilazimika kutumia mbio baada ya nyoka kuibuka katika mkutano huo wakati akijibu malalamiko ya wananchi juu ya wizara yake kutaka kupokonya ardhi yao.
Huku akiwa jukwaani waziri Maige aliwataka wananchi hao kutulia na kutaka viongozi na Wanaume waliokuwepo katika mkutano huo kusogea eneo la wan awake ambao walikuwa wakiangua vilio kwa hofu ya nyoka huyo.
"jamani naona kuna tatizo pale hebu tazamani mbona akina mama wanakimbia pale " alisema Maige huku akiendelea kuwepo jukwaani
0 comments:
Post a Comment