Home » » Mmiliki Wa Mjengwablog Akabidhi Misaada Ya Wana-Iringa Kwa Wahanga Wa Mafuriko

Mmiliki Wa Mjengwablog Akabidhi Misaada Ya Wana-Iringa Kwa Wahanga Wa Mafuriko

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
  

Pichani Mmiliki wa Mjengwablog.com na mwongozaji wa kipindi cha ' Nyumbani Na Diaspora' akikabidhi mbele ya Mwenyekiti wa kijiji cha Kisinga, Ndg. Shabani Mtimbwa na Mtendaji Kata ya Mlenge, Bi. Sarah Mbilinyi misaada iliyotolewa na Wana- iringa na watembeleaji wa mtandao wa Mjengwablog.com wakiwamo wafuatiliaji wa kipindi cha ' Nyumbani na Diaspora' kinachorushwa TBC1.

Misaada  iliyokabidhiwa ni pamoja na mahema 9 na magodoro mapya 20. Kuna mabegi mengi ya nguo na viatu vya watoto, wanawake, wanaume. Misaada ina thamani ya shilingi milioni tatu na nusu. Shukran za pekee kwa ndugu Ahmed Salim ' Asas' kwa kufanikisha lojistiki ya kufikisha Pawaga misaada hiyo.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa