Mbunge wa jimbo la Kilolo Bw Venance Mwamoto kushoto akitembelea Hospitali teule ya Ilula leo
Mwamoto akiongea na Matron wa Hospitali hiyo
Mbunge Mwamoto akitembelea mawodi ya wagonjwa Hospitali teule ya Ilula
Baadhi ya wagonjwa wakifurahia ziara za mbunge Mwamoto
Mwamoto akionyesha eneo la kuoshea maiti katika chumba cha kuhiafadhia maiti Hospitali teule ya Ilula
Mwamoto akitoa maelekezo kwa viongozi wa Hospitali hiyo kulia ni mwenyekiti wa bodi ya Hospitali hiyo Bi Anna Msola
Vitendea kazi Hospitalini hapo
Mwenyekiti wa bodi ya Hospitali hiyo Bi Anna Msola kulia akimweleza jambo mbunge Mwamoto
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Venance Mwamoto amefanya ziara ya
kushtukiza katika Hospitali Ilula ambayo ni Hospitali teule ya wilaya
ya Kilolo na kuahidi kujitolea kujenga chumba cha kuhifadhia maiti
kitakacho gharimu zaidi ya Tsh milioni 500 baada ya Hospitali hiyo
kuwa na chumba cha kuhifadhia maiti kidogo kisicho na majokofu maalum
ya kuhifadhia maiti.
Mwamoto
ambae aliambatana na mwenyekiti wa bodi ya Hospitali hiyo Bi Anna
Msolla alitembelea Hospitalini hapo leo majira ya saa 6 mchana na
kukutana na mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo kabla ya kutembezwa
maeneo mbali mbali ya Hospitali hiyo kikiwemo chumba cha kuhifadhia
maiti na mawodi ya wagonjwa .
Awali
mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr Yumpha Sovelo alimweleza
mbunge huyo kuwa Hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbali
mbali ikiwemo ya ufinyu wa chumba cha kuhifadhia maiti pia
kukosekana kwa majokofu ya kuhifadhia maiti katika chumba hicho
ambapo kwa sasa maiti zimekuwa zikilazwa chini na huwalazimu ndugu
kuchukua maiti za ndugu zao mapeni zaidi ili kuepuka kuharibika .
Pamoja
na Changamoto hiyo pia alisema suala la dawa limekuwa ni kero
kubwa kwani kiasi cha dawa ambacho wanapatiwa na MSD hakitoshelezi
mahitaji ya wagonjwa katika Hospitali hiyo ambayo hutegemewa katika
ukanda huo wa milima ya Kitonga kutokana na kutokea kwa ajali za mara
kwa mara na majeruhi kukosa dawa .
Alisema
kuwa Hospitali hiyo imefunguliwa mwaka 2007 na changamoto hiyo
imekuwepo na kuwa kwa ujio huo wa mbunge ni neema kwa wananchi wa
Kilolo ambao kutokana na kukosekana kwa chumba cha kisasa cha
kuhifadhia maiti wananchi wamekuwa wakiharakisha mazishi kukwepa
kuharibika .
Hata
hivyo alisema chumba kinachotumika sasa ni mfano wa chumba cha
kuhifadhia maiti ila kiuhalisia Hospitali hiyo haina chumba cha
kuhifadhia maiti chenye ubora .
Akielezea
suala la uhaba wa dawa alisema kuwa hali si nzuri sana kwani mfano
mwaka jana waliomba dawa za Tsh milioni 11 ila waliishia kupata dawa
za Tsh milioni 6 pekee na kwamba mgao huo wanapata kutokana na
kukosekana kwa dawa za kutosha MSD na sio pesa kwa Hospitali hiyo.
Hivyo
alisema kutokana na uhaba huo wa dawa Hospitali imekuwa ikiingia
gharama kwa kwenda kununua dawa katika maduka binafsi ambayo huuza
dawa mara mbili ya bei ya MSD .
Mbunge
Mwamoto mbali ya kupongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa kuwa
kazini wakati wote na kuendelea kuwa na mipango endelevu ya
kuboresha mazingira ya Hospitali hiyo bado alisema amesikitishwa
zaidi ya ukosefu wa chumba cha kisasa cha kuhifadhia maiti na kuwa
kwa upande wake kupitia posho zake za ubunge na ufadhili wa
wahisani wa ndani ya mkoa wa Iringa atahakikisha anajenga chumba
hicho cha kuhifadhia maiti ili kusaidia wapiga kura wake na kero
kubwa ya kufanya mazishi ya ghafla ama kutumia gharama kubwa kwenda
kuhifadhi maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa mjini Iringa .
Aidha
alisema Hospitali hiyo awali ilikuwa ni Hospitali ya kawaida chini
ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa
kabla ya serikali kuichukua na kuifanya kuwa Hospitali teule ya wilaya
na kuwa miaka 10 iliyopita akiwa mbunge alifika hapo akiwa na waziri
wa afya wakati huo Dr Hussen Mwinyi na kumwomba Hospitali hiyo kuwa
hospitali teule jambo ambalo lilifanikiwa .
Ila
alisema moja ya sifa ya kuwa Hospitali teule ya wilaya ni pamoja
na kuwa na chumba cha kuhifadhia maiti japo ilikuwa ikiendeshwa bila
kuwa na chumba hicho na wakati akiwa katika mchakato ndipo
alipopokelewa kijiti na mbunge mwenzake na hivyo kuwa nje ya ubunge na
kushindwa kujenga chumba hicho ila kwa kuwa amerudi atahakikisha
anajenga chumba hicho .
Akishukuru
kwa ahadi hiyo ya mbunge kujenga chumba cha kuhifadhia maiti
,mwenyekiti wa bodi ya Hospitali hiyo Bi Msolla alisema kuwa ujenzi
huo utakuwa ni ukombozi mkubwa kwa Hospitali hiyo na wananchi wa
Kilolo ambao wamekuwa wakifanya mazishi ya kushtukiza kutokana na
kukosekana kwa chumba cha kuhifadhia maiti .
Chanzo Matukio Daima
Chanzo Matukio Daima
0 comments:
Post a Comment