Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Aliyekuwa
mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akishuka katika
gari la polisi baada ya kufikishwa mahakamani wakati wa vurugu za
machingaji eneo la mashine tatu mjini Iringa mwaka jana(picha na
maktaba ya matukiodaima)
Na MatukiodaimaBlog
JESHI
la polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Iringa watumia
mabomu ya machozi kuwakamata wafuasi zaidi ya
60 wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema ) akiwemo
mgombea ubunge wao jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa
matatani kwa kumpiga mawe mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU)
Iringa na wananchi waliokuwa wakitoka katika mkutano wa
mgombea Urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli.
Baada
ya polisi kufatua mabamo mawili ya machozi kwa ajili ya
kusambaratisha wafuasi hao baadhi yao walikimbia huku mgombea
ubunge huyo Mchungaji Msigwa akienda kujisalimisha mwenyewe polisi
baada ya kutakiwa kufanya hivyo kabla ya kukamatwa na polisi.
Imeelezwa kuwa wafuasi
hao ambao wengi wao ni vijana walikuwa wamekutana katika eneo la
kambi ya kampeni ya Chadema iliyopo eneo la Hoteli ya Sambala
jirani na kambi ya kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kwa ajili ya kikao
cha ndani toka majira ya mchana na
jioni ndipo walipofanya vurugu hizo wakati wananchi wakitoka
katika mkutano wa kampeni za mgombea huyo wa Urais wa CCM.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa
Iringa Rmadhan Mungi aliwaeleza jana waandishi wa habari kuwa
tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12;30 jioni
baada ya wafuasi hao kufunga barabara kuu ya Iringa
–Dodoma na kufanya vurugu hizo kwa kuwarushia
mawe wananchi waliokuwa wakitoka katika mkutano wa kampeni za Dr
Magufuli uwanja wa Samora.
Alisema kuwa wakati jeshi
la polisi likiwa katika mkutano wa mgombea huyo wa Urais wa CCM
walipokea taarifa kuwa kuna vijana wa boda boda zaidi ya 150
walikuwa wakijikusanya kuelekea katika eneo hilo la Sambala Lodge na
baada ya kufuatilia ndipo walibaini kuwa wanakwenda katika kikao
chao cha ndani na kwa kawaida jeshi la polisi
halikatazi watu kufanya vikao vyao vya ndani .
“Jeshi la polisi halizuii wanachama
wa chama chochote cha siasa kufanya vikao vya ndani kwani ni haki
yao ya kisheria na kikatiba …..lakini baada ya kikao
chao kumalizika vijana hao walitoka nje ya ukumbi huo uliopo kando
kando ya barabara na kuanza kufunga barabara na kucheza muziki
katikakati ya barabara na kuzuia watumiaji wengine wa
barabara kushindwa kupita ……baada ya vurugu hizo nilimuagiza mkuu
wa FFU kwenda kuwatoa watu hao barabara ila walipuuza na kuishia
kumpiga mawe na baadae kukimbilia kujifungia katika Lodge hiyo
ya Sambala eneo ambalo wamefanya kama makao makuu ya Kampeni za
Chadema “ alisema kamanda Mungi.
Alisema wakati
wa vurugu hizo baadhi ya vijana waliumia kwa kuruka
ukuta na wengine kwa kuanguka wakati wa kujaribu kukwepa kukamatwa
na kuwa wale wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani
wakati wowote kuanzia sasa na kuwa miongoni mwao yumo
mgombea ubunge jimbo hilo Mchungaji Msigwa .
Mbali
ya mchangaji Msigwa wengine waliokamatwa kwa
tuhuma za vurugu hizo ni pamoja na mgombea udiwani kata
ya Gangilonga ambae pia ni mkuu wa kambi hiyo Dady Igogo
Kamanda Mungi alisema watuhumiwa wote watafikishwa
mahakamani wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya
upelelezi kumamilika alisema kuwa mchungaji Msigwa hakuwepo katika
eneo la tukio wakati vurugu hizo zikitokea ila ameingizwa katika
orodha ya watuhumiwa kwa wakosaji wakuu wapo makundi manne likiwemo
moja la yule anaendenda kosa kwa mikono yake ,kundi la pili
muwezeshaji au mshauri na kundi la nne kutoa hamasa kwa wakosaji
hivyo alisema mgombea huyo anashikiliwa kwa kutuma za kutoa hamasa
kwa watuhumiwa hao kufanya vurugu.
Wakati huo huo
jeshi hilo la polisi limepiga marufuku vyama vyote vya siasa
kuwahamasisha wafuasi ama wanachama wake kufanya vurugu za
wakati huu wa kampeni na kuwa kamwe jeshi hilo halitamvumilia
kiongozi ama mtu yeyote atakayejihusisha na uvunjifu wa amani.
“Amani
ni kitu cha kwanza na yeyote anayetishia kuvuruga amani ya Iringa
anatishia kazi za polisi Iringa kamwe hatavumiliwa zaidi
ya kuchukuliwa hatua kali na kuwataka vijana kuepuka kutumiwa na
wanasiasa kufanya vurugu “
Kuhusu mwenendo wa kampeni
toka zianze alisema kuwa hadi sasa tupo nusu ya
kampeni hizo toka zianze na kuwa toka tarehe 22 hadi 30 mwezi wa
nane hakukuwa na kosa lolote lililoripotiwa kutokea kuhusiana na
kampeni ila tarehe 1 hadi 5 mwezi wa tisa kulikuwa na makosa
9 yaliyoripotiwa kituoni na tarehe 5- 19 kulikuwa na makosa 17
yaliyoripotiwa na makosa 15 yalitokea jimbo la Iringa mjini na makosa
mawili wilaya ya Mufindi huku katika wilaya ya Kilolo hakuna kosa
hata moja
Hivyo
amewataka wagombea na wafuasi wao kufuata maelekezo yaliyomo katika
kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichotolewa na tume ya Taifa
ya uchaguzi .
Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo
la Iringa mjini mchungaji Msigwa katika ukurasa wake wa fecaboook
alithibitisha kukukamatwa kwa vijana hao na kiongozi wa kambi hiyo Bw
Igogo wakiwa katika ngome hiyo ya kampeni.
0 comments:
Post a Comment