Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
|
Mbunge
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akipokea fomu kutoka kwa
wazee na vijana waliomchukulia na kwenda kumkabidhi nyumbani kwake
Ibani mjini Ludewa jana |
|
Msafara wa vijana wa Boda boda zaidi ya 300 waliowasindikiza wazee wa Ludewa kumchukulia fomu mbunge Deo Filikunjombe |
|
Wazee wakimpoelekea fomu ya ubunge Deo Filikunjombe nyumbani kwake kwa maandamano |
|
Safari ya kuelekea nyumbani kwa Filikunjombe kukabidhi fomu ya ubunge |
|
Wazee hao wakiwa nyumbani kwa mbunge Filikunjombe kumkabidhi fomu ya ubunge Ludewa |
|
Hapa wakimkabidhi fomu Bw Filikunjombe |
|
Askari wa usalama barabarani akiongoza usalama |
|
Filikunjombe akielekea kuwashukuru wananchi Ludewa kwa kumchukulia fomu ya ubunge |
|
Ni zaidi ya furaha kwa mbunge Filikunjombe |
|
Kikundi cha Mganda |
|
Wananchi wakimsikiliza mbunge wao Filikunjombe |
|
Wawakilishi wa wananchi wa jimbo jirani la spika Makinda wakimpongeza Filikunjombe |
|
Filikunjombe akiwa amepokea zawadi ya mikuki kama zawadi kutoka kwa wananchi wa jimbo la Makinda ambao walifika kumpongeza pia |
|
Hapa akikabidhiwa |
|
Filikunjombe akiwashukuru kwa moyo wa upendo |
|
Mkazi wa Ludewa akionyesha furaha yake kwa mbunge |
|
Wadau mbali mbali wakimchangia pesa ya fomu Filikunjombe |
|
Filikunjombe akikabidhiwa pesa za kampeni na fomu |
|
Wananchi wakifurahia kuonyesha imani tena na Filikunjombe |
|
Filikunjombe akizungumza na wananchi hao |
|
Hotuba ya kipindi cha miaka mitano madarakani |
|
Filikunjombe na familia yake wakifurahia upendo wa wana Ludewa |
Na MatukiodaimaBLog
WAZEE
Ludewa waamchukulia fomu Deo Filikunjombe wakimwomba kuendelea
kuongoza jimbo hilo kwa miaka 20 zaidi huku wakidai kuwa kama
usingekuwa ni utaratibu wa chama cha mapinduzi (CCM) na ule wa tume
ya uchaguzi (NEC) wa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano
basi wao wangempitisha mbunge huyo bila kupingwa na uchaguzi kwa
wilaya ya Ludewa ungekuwa wa madiwani pekee na sio kwa mbunge urais Dr
John Magufuli wala mbunge wao huyo .
Mwenyewe
awaunga mkono asema anajivunia uchapakazi wa Rais Dr Jakaya Kikwete
kwani ni Rais pekee aliyesaidia kuiwezesha Ludewa kusonga mbele na
kuwa zawadi ambayo wananchi wa Ludewa wanaitoa kwa CCM ni
kuhakikisha mgombea urais wa CCM Dr Magufuli anapata kura nyingi
zaidi ukilinganisha na wilaya yoyote hapa nchini kwani pia amehusika
kuwakomboa wananchi wa Ludewa kwa kutengeneza barabara za wilaya
hiyo.
Wakizungumza wakati wa kumkabidhi fomu nyumbani kwake Ibani mjini
Ludewa wazee hao walisema wamelazimika kumchukulia fomu hiyo na
kwenda kumkabidhi baada ya kuridhishwa na kazi kubwa aliyoifanya
kwa kipindi cha miaka mitano ambayo amepata kuwa mbunge wa jimbo
hilo na kuonyesha utendaji mkubwa zaidi ukilinganisha namaendeleo
yaliyoonyeshwa na wabunge 7 waliotangulia katika jimbo hilo .
Hivyo
walisema bado wanaimani kubwa na mbunge wao na kuwa imani na
matumaini ya wananchi wa Ludewa ni kuona Filikunjombe anaendelea
kuwatumikia wananchi hao kwa vipindi vingine 4 kwa maana ya miaka
20 ama kuendelea kuongoza jimbo hilo hadi pale atakapoamua
kustaafu mwenyewe kwani utendaji kazi wake wa kazi ndio ambao
umemfanya kupewa dhamana hiyo ya kuendelea kuongoza jimbo hilo.
"
Tumekuamini na tumependezwa na utendaji kazi wako hivyo wewe
tunakubariki kuendelea kuongoza tena na tena jimbo hilo kwani
ulipokea likiwa katika hali mbaya na sasa wananchi wa Ludewa kupitia
jopo la wazee tumekuamini zaidi na tumekuchukulia fomu hii ya
ubunge kama ishara ya kukuamini zaidi ......tulikuita jembe na sasa
wewe ni katapila letu Ludewa umeweza kupita pasipo pitika
umetufanikishia maendeleo makubwa kwa kipindi kifupi zaidi "
Kwa
upande wake mbunge Filikunjombe pamoja na kuwashukuru wazee hao
na vijana wa boda boda zaidi ya 300 katika wilaya ya Ludewa
walioungana kumchukulia fomu hiyo alisema kuwa imani kubwa na
ushirikiano mkubwa ambao wananchi wa Ludewa wameuonyesha wakati wa
utumishi wake umemfariji na kuweza kufanya kazi kubwa zaidi ikiwa ni
pamoja na kuwatumikia vema buneni pasipo kusinzia kama walivyofanywa
baadhi ya wabunge wengine.
Filikunjombe
alisema ili kuwa ni vigumu kwake kusinzia bungeni kutokana na aina ya
makubaliano yake na wananchi waliomtuma kwenda kuwawakilisha na kuwa
wananchi hao walimtuma kuwasemea bungeni hivyo kama nae angeungana na
baadhi ya wabunge ambao uwakilishi wao bungeni ulikuwa ni kusinzia
basi wilaya ya Ludewa isingekuwa na maendeleo kiasi hicho.
Alisema
kuwa leo hata wale wananchi wa Ludewa ambao walikuwa wakikwepa
kuitwa wana Ludewa kutokana na uduni wa maendeleo uliokuwepo katika
wilaya hiyo hivi sasa wameanza kutembea kifua mbele kujivunia
wilaya yao tofauti na zamani ambapo wengi wao walikuwa
wakidanganya kuwa wanatoka mkoa wa Ruvuma.
"
Kazi mlionituma bungeni Dodoma nimeifanya zaidi ya uwezo wangu na
ndio maana leo wilaya yetu imepiga hatua kubwa katika maendeleo na
ukweli nimefanya yale mlionituma bungeni ombi langu kubwa kwenu
wenzangu naomba mzidi kuniombea afya njema zaidi na kuniunga mkoni
ili nikirudi bungeni tena kuweza kufanya mengine makubwa zaidi ya
haya"
Alisema
kuwa hawezi kusema wabunge waliotangulia hawakufanya chochote
kabisa katika jimbo la Ludewa japo kila mmoja aliweza kufanya kulingana
na uwezo wake ikiwa ni pamoja na mbunge wa kwanza kuleta meli ,mbunge
mwingine alileta basi ,mwingine umeme Ludewa mjini lakini kwa upande
wake amefanya zaidi ya hayo na kuifanya wilaya hiyo kuwa wilaya
ya mfano katika wilaya za mkoa wa Njombe huku akisisitiza kuwa lengo
yake ni kuona wilaya ya Ludewa inaendelea kuongoza kwa maendeleo
ukilinganisha na wilaya zote za mkoa wa Njombe.
Kwani
alisena nia, uwezo na nguvu ya kuifanya wilaya ya Ludewa kuongoza
katika maendeleo bado anayo na kuwa kazi kubwa ya wananchi wa Ludewa
kuendelea kutoa ushirikiano kwake tena .
Hata
hivyo alisema mafanikio makubwa yaliyopatikana katika wilaya hiyo
kamwe hataacha kumpongeza Rais Dr Kikwete ambae amekuwa sehemu ya
mafanikio yake na mafanikio ya wananchi wa Ludewa katika maendeleo
ila pia aliyekuwa waziri wa ujenzi Dr Magufuli ambae saa ndie Rais
mtarajiwa wa awamu ya tano kwani kati ya mawaziri waliopambana kwa
ajili ya Ludewa Dr Magufuli ni namba moja na kuwa zawadi yake ni
kupata kura za kishindo katika wilaya hiyo ya Ludewa .
Alisema
Rais Dr Kikwete kwa upande wake tayari amekwisha ahadi kufika
kuwaaga wananchi wa Ludewa kabla ya kumaliza muda wake kwa
kuzindua ujenzi wa viwanda vya chuma katika wilaya hiyo ila pia Dr
Magufuli anataraji kufika katika wilaya hiyo ya Ludewa wakati
wowote kuanzia sasa hivyo pamoja na kuwashukuru viongozi hao
wakubwa kwa upendo wao kwa wana Ludewa bado alisema historia kubwa
wameiandika katika wilaya hiyo.
Katika
zoezi hilo la wazee kumkabidhi fomu ya ubunge Bw Filikunjombe
zaidi ya Tsh 400,000 zikichangwa na wananchi mbali mbali yakiwemo
makanisa na watu binafsi pamoja na mbuzi na zawadi nyingine kama
sehemu ya kumuunga mkono mbunge huyo katika safari yake ya kugombea
tena ubunge wa jimbo hilo la Ludewa
0 comments:
Post a Comment