Home » » TIMU YA MUCOBA FC MABINGWA WA FAINALI YA KOMBE LA MUUNGANO MUFINDI 2015,MRATIBU ATANGAZA KUSTAAFU RASMI‏

TIMU YA MUCOBA FC MABINGWA WA FAINALI YA KOMBE LA MUUNGANO MUFINDI 2015,MRATIBU ATANGAZA KUSTAAFU RASMI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkuu  wa  wilaya ya Mufindi Mboni Mhita katikati  akiwa katika picha ya pamoja na   mabingwa wa mashindano ya  kombe la Muungano Mufindi timu ya Mucoba Fc ,wa kwanza kulia ni mratibu wa mashindano hayo aliyestaafu rasmi Daud Yassin na mdau mkubwa wa  soka mkoa wa Iringa Feisal Asas
Mkuu wa wilaya ya  Mufindi Mboni Mhita  akikabidhi kombe kwa mabingwa  timu ya MUcoba FC
Mkuu wa wilaya ya  Mufindi Mboni Mhita  akikabidhi kombe kwa mabingwa  timu ya MUcoba FC
Mratibu  wa kombe la Muungano Mufindi Daud Yassin akitangaza  kustaafu   nafasi yake hiyo
Mabingwa wa mashindano ya  kombe la Mungano Mufindi
washindi  wa  pili wa mashindano ya  kombe la Muungano Mufindi timu ya Dodoma Academ  wakipita kuvishwa medali na Feisal Asas

Mwalimu  wa  timu ya Mabingwa  wa fainali ya Muungano Cup akipongezwa


Na  MatukiodaimaBlog 
MASHINDANO  ya  kombe la  Muungano Mufindi yamefikia tamati baada ya  timu ya benki ya  wananchi wilaya ya  Mufindi  (MUCOBA FC) kuibukwa mabingwa  wa  fainali ya mashindano hayo kwa kuigagadua (kuifunga) timu ya Academ kutoka Dodoma kwa  jumla ya magoli 2-0

 Huku  mratibu  wa mashindano  hayo  Daud Yassin akitangaza  kustaafu  rasmi nafasi  yake  hiyo   baada ya  kuitumikia kwa miaka 19  hivi  sasa .

Mratibu  huyo  aliweza  kuwaaga rasmi  wapenzi wa mpira wa miguu katika wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa baada ya  kumalizika kwa mchezo huo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa  wa  shule ya msingi wambi mjini Mafinga
 
. Yassin aliwashukuru  wadau  wote wa soka  waliomsaidia kwa namna moja  au nyingine kwa  miaka  19  aliyoratibu  mashindano  hayo.

 Alisema pia anawashukuru  viongozi mbalimbali, chama cha soka  wilaya ya Mufindi, chama cha soka mkoa wa lringa, shirikisho la soka nchi TFF, na ZFA kwa  kuonyesha ukaribu  wao kwa  kipindi  chote cha mashindano  hayo .

Pia  aliwaomba  radhi wadau  wote  ambao walikwazika kwa utendaji  wake endapo alikosea  katika utendaji wake na kuwa haikuwa makusudi  yake  kuwakwaza .

Amesema  kwa sasa hatajihusisha  na mambo ya soka  tena katika  wilaya  hiyo kwani kazi  aliyoifanya kwa  kipindi cha miaka  hiyo 19  ni  kubwa na wilaya ya  Mufindi na mkoa wa Iringa umetangazwa  zaidi  kupitia mashindano  hayo .

" Nimejifunza mengi mwaka huu mambo yalikuwa magum sana japo anawashukuru  wale waliomsaidia kufanikisha na kuwa atawaandikia rasmi kuwashukuru.....Wakiwemo  viongozi wa kisiasa mbunge  wa kaskazini  Mahamudu Mgimwa na mjumbe wa NEC na mwenyekiti  wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini  kwa  kumsaidia  kufanikisha mashindano hayo kwa  mwaka huu "

Mgeni  rasmi katika fainali  hiyo mkuu  wa  wilaya ya  Mufindi Mboni Mhita  mbali ya  kumshukuru mratibu  huyo wa kombe la Muungano Mufindi  ,Yassin  pia alipongeza  wadau  wote  ambao  wameyafikisha hapo mashindano  hayo na kuwa  wilaya ya Mufindi  imeweza  kutangazwa  vilivyo kupitia  soka .

Hivyo aliwataka  wadau wa soka  wilaya ya  Mufindi  kuangalia  uwezekano  wa  kuendeleza mashindano  hayo  baada ya  mratibu  wake  kustaafu  rasmi na kuwa  akiwa  mkuu wa wilaya  hiyo atahakikisha mashindano hayo yanaendelea  japo  ushauri  wa mratibu  huyo  utaendelea  kuhitajika  zaidi.

 Katika  mashindano  hayo mshindi  wa kwanza  timu ya Mucoba Fc  ilipata  zaiwa ya kombe  kubwa , pesa taslim kiasi cha Tsh  milioni 5 ,jezi  seti  nne na medali ,wakati mshindi  wa pili Dodoma Academ ikipata  kiasi cha Tsh milioni 2.5 ,seti tatu za  jezi  pamoja na medali  wakati mchezaji  bora  akipata kiasi  cha Tsh 500,000

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa