Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Makatibu kata wa CCM jimbo la Isimani wakiwa wamezunguka pikipiki 16 zilizotolewa na mbunge wao Wiliam Lukuvi kwa ajili ya kuwasaidia katika shughuli za kila siku |
makatibu kata na katibu wa wilaya ya Iringa wakishangilia wakati katibu wa mkoa wa Iringa Hassan Mtenga akijaribu pikipiki hizo |
katibu wa mbunge wa jimbo la Isimani Bw Thom Malenga kushoto akimkabidhi simu 16 zilizotolewa pamoja na pikipiki 16 na mbunge Lukuvi kwa ajili ya makatibu wa CCM kata |
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga akikabidhi simu kwa katibu kata wa CCM jimbo la Isimani |
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi emekabidhi msaada wa pikipiki 16
zenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 22 makatibu kata wote 16 wa chama
cha mapinduzi (CCM )katika jimbo hilo la Isimani wilaya ya Iringa
vijijini ili kuwawezesha kufanya kazi ya chama kiufanisi zaidi .
Akikabidhi
msaada huo pikipiki na simu 16 leo kwa makatibu hao wa kata kwa niaba ya
mbunge Lukuvi ,katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw Hassan Mtenga alisema
kuwa mkoa wa Iringa una zaidi ya wabunge wa watano wanaotokana na
chama cha CCM ila hajapata kuona mbunge anayewajali makatibu wa chama
kama alivyofanya mbunge huyo wa jimbo la Isimani na kuwa kufanya
hivyo ni kuongeza ushindi wa CCM .
"
katika mkoa wetu wa Iringa tunaowabunge wa CCM lakini toka
wameanza mbaka wanamaliza hawajapata kutoa msaada kama huo ila
Lukuvi si tu anaanza leo tuseme ni muendelezo kwa ni mara kwa mara
amekuwa jirani na chama kwa kusaidia makatibu hao usafiri wa
pikipiki na kuwa hii ni mara ya pili anatoa msaada huo wa pikipiki
baada ya zile za awali kuchakaa"
Bw
Mtenga alisema kuwa Lukuvi amekuwa ni mbunge na kiongozi wa aina
yake kwani amekuwa ni msaada mkubwa zaidi ndani ya chama na hata
serikalini kutokana na utendaji kazi wake na hivyo mbali ya kuwa si
wakati muafaka sana ila yeye kama katibu wa CCM mkoa wa Iringa
anatambua mchango mkubwa na heshima kubwa ambayo mbunge Lukuvi
ameonyesha ndani ya chama na katika jimbo lake la Isimani kwa
kutekeleza ilani vizuri na hivyo kuwataka makatibu hao na wana CCM
jimbo la Isimani kuendelea kutoa ushirikiano kwa mbunge wao.
"
Mimi ni katibu wa CCM mkoa hivyo natamka wazi kuwa mbunge Lukuvi
aendelee kuwa mbunge wa jimbo la Isimani kwani ni mbunge anayetambua
changamoto za watendaji wake na wananchi waliomchagua na kuzitatua na
ndio jambo ambalo chama kinahitaji kwa wabunge wake kuzifanya "
Katibu
wa CCM wilaya ya Iringa Bw Andrew Kashililika alisema kuwa msaada huo
wa piki piki katika jimbo la Isimani ni msaada mkubwa zaidi kwani
hali ya usafiri kwa makatibu wa CCM kata bila jitihada za mbunge huyo
hali ya utendaji kazi kwao ingekuwa ngumu zaidi.
katibu
huyo alisema ushindi ambao CCM iliupata katika uchaguzi wa Serikali
za mitaa kwa CCM kushinda zaidi ya asilimia 90n katika wilaya hiyo ya
Iringa vijijini ni wazi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba
mwaka huu CCM kitaibuka na ushindi wa kishindo zaidi .
Kwa
upande wake katibu wa ofisi ya mbunge Lukuvi Bw Thom Malenga
alisema kuwa ofisi ya mbunge ilipokea barua za maombi kutoka kwa
makatibu hao wa CCM kata kuomba kupewa pikipiki mpya baada ya zile
za awali kuchakaa na hivyo kukwamisha utendaji kazi wao .
Alisema
kuwa baada ya hapo ndipo Lukuvi alipoamua kutafuta pesa kiasi cha
Tsh milioni 26 kwa ajili ya kununua pikipiki hizo na kuwapa mawasiliano
ya simu baada ya kuwa sehemu kubwa ya jimbo hilo kuwa na
mawasiliano ya simu na kutokana na kuwa na vitendea kazi vya
mawasiliano itawawezesha kufikisha taarifa kwa haraka katika makao
makuu ya chama.
Hata
hivyo aliwataka makatibu kata hao kujaribu kuwa waangalifu katika
kutumia pikipiki hizo ili kuepuka kuwasababishia ajali kwani bila
uangalifu katika matumizi upo uwezekano wa badala ya kufurahia
msaada huo wakaishia kujutia majeraha yatakayotokana na wao kutokuwa
makini.
Bw
Zacharia Kitule katibu kata wa CCM kata ya Nyang'oro akishukuru kwa
niaba ya wenzake kwa msaada huo alimpongeza mbunge Lukuvi kwa
kuwamsikivu na kutimiza kila anachoahidi kwa wakati zaidi na kuwa wao
kama makatibu kata wapo tayari kuendelea kutoa ushirikiano zaidi
kwake ili kuona anaendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo hadi hapo
atakapoamua kustaafu mwenyewe.
0 comments:
Post a Comment