Home » » FILIKUNJOMBE AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUTOWASAHAU WANANCHI WALIOWACHAGUA

FILIKUNJOMBE AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUTOWASAHAU WANANCHI WALIOWACHAGUA


Mbunge wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akitoa  salama  za  pore kwa  wafiwa  wakati wa mazishi ya MNEC wilaya ya  Ludewa  Elizabeth Haule
Mchumi  wa  UWT  mkoa  wa Njombe Dr  Suazana  Kolimba  akitoa  salam  zake 
katibu  wa  CCM  Ludewa  Lusiana Mbossa akimsikiliza DR  Kolimba
katibu  wa CCM Ludewa Bw Mbossa kushoto  akimkaribisha  mbunge  Filikunjombe kutoa  salam  zake
Mbunge  Filikunjombe  akiwaasa  wana siasa kuwajali  zaidi  wananchi
Mwenyekiti  wa Halmashauri ya  Ludewa Bw  Kongo  akiweka  shada la maua
 DC  Ludewa  Juma Madaha  akiweka  shada la maua

Katibu wa CCM  wa  mkoa  wa Njombe Bw  Hosea Mpagike akiweka shada la maua
Mwwenyekiti  wa CCM Ludewa  Bw  Stanley Kolimba  akisogea kuweka shada la maua
Viongozi  wa Chama  na  serikali  Ludewa wakiwa  katika mazishi  hayo
Ibada  ya  mazishi
Vijana  wa CCM  wakiwa  wamebeba  jeneza lenye mwili wa MNEC Ludewa  Elizabeth Haule
katibu  wa  kundi la Sanaa Ludewa na mwanahabari Nickson  Mahundi  akiweka shada la maua

Na MatukiodaimaBlog

MBUNGE wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  amewataka  viongozi  wa  kisiasa  kuweza  kujitafakari juu  ya nafasi  wanazoziongoza ili  kuona kama  wapo kwa  ajili yao  binafsi ama  kwa ajili ya jamii  iliyowachagua.

Filikunjombe alitoa  kauli   hiyo jana  wakati  akitoa  salam   zake  za  pore kwa  wakazi  wa  Ludewa katika mazishi ya  aliyekuwa  mjumbe  wa halmashauri  kuu ya  Taifa (NEC) wilayani  hapo Elizabeth Haule yaliyofanyika  kijijini kwake  Luana ,  kuwa lazima  viongozi  kujenga  utamaduni  wa  kuwatumikia  wananchi  ambao  wamewawezesha   kuwa na nafasi  hizo  badala  ya  kujinufaisha    wao.

Mbunge Filikunjombe  alisema  kuwa  wilaya ya  Ludewa  imempoteza kiongozi imara  na  kuwa  uongozi  wa MNEC  huyo  ulikuwa ni  wa kuigwa  kutokana na namna  ambavyo alivyokuwa  akiwasilisha mambo  yake  na  siku   zote  kuonyesha  kuwatumikia   wana CCM waliomuwezesha   kuwa   MNEC.

" Siku  mbili kabla ya  kifo  chake  nilipata  kuzungumza na marehemu  kupanga   juu ya sherehe  ya CCM ila  alinikumbusha   juu ya barabara ya  Malato ,Itundu alikuja  kwangu na  kuniomba kila  wakati .....hadi  siku ya  mwisho nikipangana  nae mwishoni  aliniuliza  ahadi yake  juu ya barabara    vipi  na  siku  moja  nilimtania  kuwa wewe  ni mkazi  wa Malato na  unasali Anglicana na  ile  barabara  inakwenda kanisa la Roman Katoliki ila  alisema  wote ni  watu  wake ....hivyo  naomba  nisema  siwezi kuacha  kutekeleza ombi lake  la barabara"

Mbunge   huyo  alisema  kuwa  amepata   kujifunza  mengi  kutoka kwa marehemu  huyo  enzi  za uhai alikuwa  akiomba   pasipo  kutumia nguvu na  moja kati ya  jambo  ambalo  alikuwa  akimuomba ni  pamoja na  kusaidia  kuchonga barabara ya  kijiji  hicho  kuelekea kanisa la  RC lililopo  umbali wa  zaidi ya  Kilometa 5  kutoka  barabara  kuu ya  Ludewa - Njombe .

"  Mimi  pia  nimepata  kujifunza  kutoka kwa marehemu  huyo  kumbe unaweza  kuomba bila kutumia  nguvu  zaidi na  ukapata  ....suala  hili la kuniomba  kusaidia  kuchonga  barabara  kila  wakati  amekuwa  akinipigia   simu na  kuniomba  lakini  naomba  kutamka  leo  hapa  kuwa nitamuenzi kwa  kutengeneza  barabara   hiyo ambayo  hakuna  hata  mwananchi  mmoja  amepata  kuniomba barabara   hiyo  itajengwa  mwezi  wa sita  na  pia  nitasogeza  umeme kutoka  Malato kwenda kitongoji  cha Itundu kuanzia  mwezi  wa tano  mwaka huu"

Alisema  kuwa  marehemu  alikuwa akiutumia uongozi  wake  vizuri  kwa  kuwajali  wananchi  wake  hivyo  ni  vema  kila  kiongozi wa kisiasa   kuona  anatumia  vema nafasi   yake  aliyopewa na  wananchi  kwa kuwatumikia  waliomchagua.


Aidha   alisema  kuwa  kwa  upande  wake  bungeni  akiwa anaomba  jambo  kwa ajili ya  wana  Ludewa siku  zote  amekuwa  akitumia  nguvu lakini  marehemu   yeye  alikuwa  akiomba kwa  unyenyekevu  na  siku  zote  alikuwa ni  mtu  wa  kuwatumikia  wananchi  wake hivyo lazima  kila  kiongozi  wa siasa  kujitafakari  zaidi .

Marehemu  Haule  katika  uhai  wake  mbali ya  kuwa mjumbe wa NEC Taifa  akiwakilisha  wilaya ya  Ludewa  pia  alikuwa ni mwenyekiti  wa UVCCM  wilaya  ya  Ludewa na mwenyekiti  wa kikundi  cha  Sanaa  Ludewa   alifariki kwa  ugonjwa wa moyo juzi  katika  Hospitali ya  wilaya ya  Ludewa baada ya  kuzidiwa toka  jumapili  akitokea  katika  sherehe za  miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Powered by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa