Na matukiodaimablog
WAZAZI
wa wanafunzi wanaosoma shule ya Kimataifa ya Southern Highlands
Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamechangia kiasi cha
zaidi ya Tsh milioni 5 kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za
uongozi wa shule hiyo kuanzisha shule ya sekondari inayojulikana
kwa jina la Mufindi Highlands School.
Michango
hiyo ambayo ni fedha taslimu na ahadi ilitolewa jana wakati wa
mahafali ya chekechea na siku ya wazazi shuleni hapo kufuatia
wazazi hao kuvutiwa na taarifa ya mkurugenzi wa shule hiyo kuhusu
uanzishwaji wa shule mpya ya sekondari .
Mmoja
kati ya wazazi hao Blankson Ponela ambae alijitolea ahadi ya
kuachangia kiasi cha Tsh milioni 1.5 alisema kuwa amevutiwa zaidi na
jitihada za uongozi wa shule hiyo kwa kuanzisha shule ya
sekondari yake.
Kwani
alisema kuwa awali wanafunzi wanaofaulu katika shule hiyo
wamekuwa wakipata wakati mgumu kuzoea mazingira ya shule za
sekondari ambazo wanafunzi wake wametoka katika shule za msingi
za serikali ambao uwezo wao huwa na chini ya ule wa wanafunzi
waliotoka katika shule hiyo ya Southern Hihglands ambayo wanafunzi
hujifunza lugha mbali mbali ikiwemo ya Kiingereza na kifaransa na
Kiswahili .
"Tunapenda
kuupongeza uongozi wa shule hii kwa kuja na wazo la kuwa na shule
ya sekondari yake ambayo itawachukua wanafunzi wanaofaulu katika
shule hii ya msingi .......binafsi na familia yangu kwa ajili ya
kuunga mkono hili ninaahidi kuunga mkono kwa kuchangia kiasi cha
Tsh milioni 1.5 ili kufanikisha ujenzi huo"
Huku
Bw Peter Ole Mamasita alisema kuwa kwa mkoa wa Iringa shule hiyo
ya Southern ndio imeendelea kuwa shule yenye rekodi nzuri ya
ufaulu wa wanafunzi ukilinganisha na shule nyingine za binafsi na
serikali .
Hivyo
alisema kuanzishwa kwa shule hiyo ni imani kubwa kwa wazazi
katika wilaya ya Mufindi na nje ya wilaya hiyo kuendelea kunufaika
na matunda ya shule hiyo hasa kwa kuendelea kuwafanya watoto wao
kupata elimu ya chekechea ,msingi hadi sekondari wakiwa katika
eneo moja badala ya kuanza kutafuta shule nyingine nje ya wilaya
hiyo.
Mkuu
wa shule hiyo Joson Nyabuto alisema kuwa shule hiyo kwa huu
2014 ilikuwa na wanafunzi 48 na wote
walifaulu kujiuga na sekondari na kuifanya shule hiyo katika matokeo
ya mtihani huo kitaifa kwa wilaya kushika nafasi ya kwanza kati ya
shule 167 kimkoa nafasi ya nane kati ya shule 458 na kitaifa kuwa
shule ya 353 kati ya shule zaidi ya 15,867 hivyo kwa matokeo hayo
shule hiyo imeweza kupanda kwa wastani wa pointi tano zaidi ya mwaka
jana .
Alisema kwa mwaka jana shule hiyo ilifaulisha pia wanafunzi wote 47 na kushika nafasi ya pili
kiwilaya nafasi ya 9 kimkoa na kitaifa kuwa shule ya 288.
Mkurugezi
mtendaji wa shule hiyo Mary Mungai alisema kuwa ujenzi wa
shule hiyo kwa awamu ya kwanza unategemea kugharimu kiasi cha Tsh
milioni 50 kwa kujenga mabweni mawili kwa ajili ya wavulana na
wasichana pamoja na madarasa manne na nyumba moja ya mwalimu .
Aliwaomba wadau mbali mbali wa ndani ya nchi na nje ya nchi kusaidia ujenzi huo wa shule ya sekondari kwa kuchangia michango yao kwa M-Pesa 0754651966 ama 0752840884 kwani alisema upatikanaji wa fedha hizi ni mgumu zaidi iwapo ataufanya peke yake ila kama wadau mbali mbali wataunganisha nguvu zao uwezekano wa kumaliza ujenzi huo kwa wakati upo.
Hata
hivyo alisema awamu ya pili itakuwa ujenzi wa maabara ya kiasasa
,kuongeza nyumba vya madarasa ,nyumba za walimu na kuwa shule
hiyo inatarajiwa kujengwa kwa awamu tatu hadi kukamilika kwake na
jumla ya Tsh bilioni 1 ndizo zinahitajika ili kukamilisha ujenzi
wa shule hiyo ya sekondari japo alisema mchakato wa kuanza
kupokea wanafunzi kwa ajili ya kuanza kidato cha kwanza utaanza
mapema mwaka huu na mwakani shule hiyo ya Southern Highlands
Mafinda itakuwa pia na wanafunzi wa kidato cha kwanza kupitia shule
yake ya sekondari ya Mufindi Highlands School
Mkurugenzi huyo alisema kwa wazazi wanaotaka watoto wao kujiunga na shule hiyo nafasi za masomo kuanzia chekechea , darasa la kwanza hadi la tatu wanaotokea
kiswahili medium schools na la tano pia wakati ,Darasa la 4 na 6 wanaotoka English medium.
Huku wale wa la nne na sita wale
wanaotoka English medium schools wanaweza kujiunga na shule hiyo kwa kujaza fomu za kujiunga
zinazopatikana shuleni Mafinga na kutakuwa na interviews tarehe 13 / 12/2014
maeneo yafuatayo. Shuleni Southern Highlands Mafinga, Oyster Bay
Primary school, Dar es
salaam, chuo cha Nursing Ilembula na Misufini primary school, Songea
ama kuwasiliana na uongozi wa shule kwa simu hii 0756749151 au
0754651966
Pia alisema sekondari form one wanazo nafasi na jina la sekondari; Mufindi
Highlands School
Alisema kuwa shule hiyo ni moja kati ya shule bora katika wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa pamoja na Taifa na kwa kuwa toka ianzishwe kwake haijapata kufelisha hata mwanafunzi mmoja zaidi ya kufaulisha wanafunzi wote darasa la saba .
|
0 comments:
Post a Comment