Home » » JIWE GANGLONGA LINAVYOUTANGAZA MKOA WA IRINGA

JIWE GANGLONGA LINAVYOUTANGAZA MKOA WA IRINGA

 Jiwe la Gangilonga -Iringa
 Muonekao wa mtaa wa Gangilonga kutokea juu ya jiwe gangilonga.

Mji wa Iringa


Na Iringa yetu Blog
Mkoa wa Iringa ni moja kati ya mikoa 30 ya Tanzania.
Jiografia
Mkoa wa Iringa uko katika Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania. Mkoa huu unapakana na ukanda mkavu wa kati wa Tanzania katika upande wa kaskazini na kupakana kusini na Ziwa Nyasa. Mkoa wa Iringa umetanda kati ya latitudo 7º 05˝ na 12º 32˝ kusini, na longitude 33º 47˝ hadi 36º 32˝ mashariki mwa Meridian. Ziwa Nyasa linatenganisha Mkoa wa Iringa na nchi ya Malawi upande wa kusini Magharibi mwa Tanzania.
Mkoa wa Iringa una eneo lenye ukubwa wa jumla ya km 58,936. Wastani wa asilimia 74 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za kilimo ambalo ni sawa na km² 43,935. Eneo linalobakia la km2 15,001 ni eneo la maji, hifadhi ya mbuga za wanyama, milima na misitu.
Wakazi
Mwaka 2002 palikuwa na wakazi 1,495,333 [1] katika wilaya zifuatazo: Iringa Kijijini (wakazi 245,623), Mufindi (wakazi 283,032), Makete (wakazi 106,061), Njombe (wakazi 420,348), Ludewa (wakazi 128,520), Iringa Mjini (wakazi 106,668), na Kilolo (wakazi 205,081).
Makao makuu yako Iringa mjini.
Wenyeji wa mkoa ni hasa kati ya makabila yafuatayo: Wahehe, Wabena, Wakinga, Wapangwa na Wawanji.
Mwaka 2010 mkoa umemegwa na kuzaa mkoa wa Njombe upande wa kusini.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Iringa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa